Makamba ataka kupambana kwa pamoja ili kumaliza changamoto za Lushoto

 Mbunge wa Jimbo la  Bumbuli  Mkoani Tanga January Makamba amesema wilaya ya Lushoto bado ina changamoto za kimaendeleo ambazo zinaitaji  umoja na ushirikiano ili kuzimaliza kwa haraka.

Hayo ameyasema wakati wa  Uchaguzi wa wenyeviti  wa Halmashauri  za Bumbuli na Lushoto uliofanyika katika ukumbi wa CCM wilayani humo.

 Makamba ambaye pia ni Katibu mstaafu wa Halmashauri kuu ya Taifa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) alisema  suala zima la maendeleo wilaya ya lushoto imechelewa kidogo  kwani  maeneo mengi  umeme, maji  na barabara bado  huduma hiyo haijawafikia wananchi hivyo silaha  ya kuweza kuwahi kwenye maendeleo ni umoja na sivinginevyo .

"  silaha  ya mafanikio ya kuwafikia wenzetu kwenye maendeleo ni moja tu ambayo ni kupambana kwa pamoja ,tuseme  kwa sauti moja kwani hata sisi bungeni agenda za milimani tunazisukuma kwa pamoja Mimi na Wabunge  wenzangu "Alisma Makamba

Alisisistiza kuwa Maendeleo ni mapambano  na ni harakati  nakwamba Madiwani na Wabunge  ndo askari wa mstari wa Mbele  kwenye harakati  hizo za maendeleo.

Makamba  alitumia  fursa hiyo kuwataka Madiwani wavunje makundi baada ya kuwapata wenyeviti  na viongozi wengine waliowachagua ili wawe kitu kimoja katika kufanya kazi za kutafuta maenedeleo ya wananchi.

" Baada ya Uchaguzi leo kusitokee vikundi vikaanza kunongona pembeni kuwa bora katushinda kwenye kura basi ngoja tuone uo uenyekiti wake " Kama vitatokea  vitakuwa  vinahujumu maendeleo na Chama chetu  hivyo vikitokea vikundi hivyo basi viongozi wasisite kuvichuliwa hatua  japo siwafundishi kazi viongozi wangu" Alisisistiza Makamba .

Amir Shehiza ambaye amechaguliwa  kuiongoza Halmashauri ya Bumbuli kwa kipindi  pili amesema mara baada ya kuapishwa  ataanza kufufua vyanzo vya mapato vilivyopo ndani ya Halmashauri ya bumbuli ili wapunguze changamoto ya mapato ambayo walikuwanayo ikiwemo kwenda ngazi za juu kuomba kufunguliwa kwa kiwanda ambacho kilikuwa kinawaingizia kwa mwaka mili.80.

Kwa upande wake Mwenyekiti Mteule wa Halmashauri ya lushoto Methew Mbaruku alisema yeye ataanza kuisimamia halmashauri ili iweze kutoa asilimia 10 kwa wakati  kwa vijana na wanawake

Mkurugenzi wa Uchaguzi huo wa wenyeviti Ramadhani Mahanyu alisema kuwa Uchaguzi ulikuwa huru na wa uwazi nakwamba nafasi zilishindaniwa ilikuwa ni nafasi ya uenyekiti ,Umakamu wenyekiti na ukatibu wa Madiwani  Uchaguzi huo ulikuwa ni wa Halmashauri zote mbili za Bumbuli na Lushoto kwa nafasi zote hizo.

No comments: