WANAFUNZI 490,103 WANATARAJIWA KUFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE KESHO
JUMLA ya Wanafunzi 490,103 wanatarajiwa kufanya mtihani wa Kidato cha Nne kesho Novemba 22 ambapo wavulana ni 213,553 sawa na asilimia 47 huku wasichana wakiwa ni 234,103 sawa na asilimia 52.3.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais-Tamisemi, kati ya wanaotarajiwa kufanya mtihani huo watahiniwa binafsi ni 41,939 wavulana wakiwa 18,118 sawa na asilimia 43.2 n wasichana ni 23,821 sawa na asilimia 56.8.
Wanafunzi wenye uhitaji maalum ni 893 ambapo 425 kati yao ni wenye uoni hafifu, 60 wasioona, 186 viziwi na 222 walemavu wa viungo.
Katika kundi la watahiniwa binafsi wanafunzi wenye mahitaji maalum kwenye kundi hilo ni 11 ambapo saba kati yao wana uoni hafifu na wanne ni wasioona..
Mwaka 2019 wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne walikua ni 485,866 hivyo mwaka huu kuna ongezeko la asilimia 0.9.
Kuhusu mtihani wa maarifa (QT) jumla ya wanafunzi 9,426 wanatarajiwa kufanya mtihani huo ambapo wavulana ni 4,147 sawa na asilimia 44 na wasichana ni 5,279 sawa na asilimia 56. Katika kundi hili waliofanya mwaka 2019 ni 12,984.
No comments: