SEKTA YA UVUVI KUIMARIKA KWA KIPINDI CHA MIAKATA MITANO IJAYO-SERIKALI

 Na Mwaandishi wetu Mtwara

SERIKALI imesema kwa kipindi cha miaka mitano ijayo itahakikisha sekta ya uvuvi inaimarika kwa kuboresha mazingira ikiwemo matumizi ya sayansi na tecknolojia ya uvuvi endelevu.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa  amesema haya mkoani hapa wakati akifunga sherehe za maadhmisho ya uvuvi duniani yaliofanyika mkoani. Sherehe hizo ziliandaliwa na Muungano wa Kitaifa wa Uvuvi wa Jodari Tanzania.

“Kwa kipindi cha miaka mitano ijayo serikali itahakikisha sekta ya uvuvi inaimarika kwa kuongeza matumizi ya sayansi na technolojia ya uvivu endelevu, ili kuwezesha mauzo ya bidhaa za uvuvi nje ya nchi, kuchangia zaidi katika uchumi wa taifa,” amesema

Katika risala iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Danstan Kyobya, Mkuu wa mkoa huyo alisema pia kwamba uimarishwaji wa sekta ya uvuvi utasaidia kuzalisha ajira kwa vijana, kuboresha maisha ya wavuvi na wanacnhi kwa ujumla haswa watu wa mtwara wanaozungukwa na bahari.

Byakanwa amewataka pia wadaum mbalimbali wakiwemo Tuna Fisheries National Alliance Tanzania kuunga mkono serikali kwa kubuni mradi wa bandari ya uvuvi kwa kuweka vivutio kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi na kutekeleza kanuni na sheria ya kusimamia bahari.

Pia amewataka kuungana na serikali katika kuhamasisha matumizi ya zana bora, kuimarisha miundombinu na technolojia, kuhifahi mazalia na kuendelea kuhifadhi mazingira na mazalia ya smakia ili kuhakikisha uzalishaji wenye tija kwa wavuvi na taifa kwa jumla.

Mkuu huyo pia aliwata TUNA Alliance kuhamasisha wananchama wake kuanzisha na kuimarisha vikundi na vyama vya ushirika kwa lengo la kuwpatia ujuzi, vifaa na zana bora za uvuvi.

“Mkoa wa Mtwara umeboresha miunodbinu yake ya umeme, barabara, bandari na kiwanja cha ndege, ambayo inawahakikishia wavuvi wa jodari na wengineo mazingira wezeshe na uwekezaji na kuifanya Mtwara kuwa langi kuu la uchumi la nchi yetu,” amesema.

Wakati huo huo, Kyobya amewata maafisa uvuvi na wasaidizi wake kuacha mara moja kukaa maofisin na badala yake watoke na kuwatembelea, kusikiliza na kutatua changamoto na kero zinazowakabili wavuvi na wafanyabiashara wilyani Mtwara.

Pia amewataka kuhakikisha wavuvi wote wanapewa lessen za uvuvi ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za uvuvi na kukagua vyombo vya wavuvi hao.

“Hakikisheni mnakagua vyombo vya wavuvi wote na kuweka mikakati ya kuweka mazingira bora ya wafanyabiashara na wavuvi,” amesema.


 Mkuu wa Wikaya Danstan Kyobya akipokea zawadi wa samaki aina ya jodari kutoka kwa mmoja wa wavuvi waliohudhuria Sherehe za maadhimisho ya siku ya uvuvi duniani







Akitembelea soko la samaki feri baada ya kufunga sherehe za maadhimisho ya siku ya Uvivu dunian




No comments: