UKUAJI WA MIJI NA HAJA YA KUELEWA MAZINGIRA YA WATOTO NA VIJANA


UKUAJI wa kasi wa miji nchini Tanzania kuna hitaji uelewa mazingira yanayosibu watoto katika miji hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya ESRF DktTausi Kida wakati akitoa maneno ya ukaribisho wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kujadili na ukusanyaji wa maoni ya wadau mbalimbali kuhusu ukuajiwa miji na athari zake kwa watoto.
Kwa mujibu waDkt Kida kundi hilo la watoto na vijana ndio wanaotengeneza hali ya badaae ya maendeleo yaTaifa.  Moja ya tatu ya watanzania, kiasi cha watu milioni 23, wanaoishi katika miji wapo chini ya miaka 18.
“ Vijana hao wanapoelekea utu uzima wanakumbana na matatizo mengi ya kijamii na kiuchumi, matatizo ambayo kama yasipoangaliwa na kupatiwa ufumbuzi yanadhuru maisha yao ya baadae” anasema Dkt. Kida.
Dkt. Kida alisema katika hotuba yakekwamba kwa kuangalia miji ya Dar es salaam na Mwanza  unaona kwamba sirahisi kutambua changamoto na pia fursa zilizopo kutokana na ukweli kuwa hakuna takwimu za kutosheleza mahitaji ya uchambuzi wa mazingira yanayogusa watoto hao.
Anasema kutokana na haja hiyo, kongamano hilo la kwanza limelenga kuleta pamoja wadau wote kuzungumzia masuala hayo na kuyapatia muundo bora wa ufumbuzi kwa lengo la kushauri watunga sera.
Pamoja na kueleza nia ya mkutano Dkt.  Kida pia alishukuru Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa(UNICEF) Tanzania kwa  kuwa mshirika mzuri katika mradi huo ambao upo ndani ya mradi wa Maabara ya Miji Tanzania (TULab) ambao ESRF wametengeneza ramani ya utekelezaji wa maendeleo ndani ya miji. 
Aidha alishukuru Wizara ya Fedha na Mipango naTamisemi kwa kuwezesha kuwapo kwa tathmini ya watoto na vijana wa mijini.
TULab ni sehemu katika mpango wa kuendeleza miji katika ilivyoainishwa katika Mpango wa pili wa Maendeleo ya Taifa 2016/17 – 2020/21
Kwa mujibu wa Dkt.  Kida,TULab inaendelea kusaidia juhudi za kitaifa za utengenezaji wa sera na kutambua athari zinazokabili miji ya Tanzania.
Akifungua mkutao huo Dkt. Mukuki Hante, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Miji kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) alisema kwamba Tulab ni jukwaa ambalo linasaidia serikali kuona maendeleo ya miji na athari zake na namna ya kujipanga.
Alisema mkutano huo ni muhimu kwa kuwa unajazia tatizo la watoto na fursa zao katika ukuaji wa miji.

Aliwataka wajumbe kutoa mawazo ili kusaidia utengenezaji mpango wa uchambuzi masuala ya watoto na vijana katika miji.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho wakati wa mkutano wa kujadili ukuaji wa miji na athari zake kwa watoto uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya miji Wizara ya Tamisem, Dk Mukuki Hante akifungua mkutano wa kujadili ukuaji wa miji na athari zake kwa watoto uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene akielezea mradi huo wakati wa mkutano wa kujadili ukuaji wa miji na athari zake kwa watoto uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Dk Audax Kweyamba akizungumzia haki ya watoto ya kucheza na kushiriki maisha ya mijini wakati wa  mkutano wa kujadili ukuaji wa miji na athari zake kwa watoto uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Dk Rehema Mzimbiri akizungumzia masuala ya usalama wa chakula na lishe miongoni mwa watoto na vijana katika miji wakati wa mkutano wa kujadili ukuaji wa miji na athari zake kwa watoto uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Bw. Joseph T. Baitwa (kushoto) akizungumzia masuala ya ulinzi kwa watoto na vijana dhidi ya ukatili wa kijinsia, kunyonywa na kususwa wakati wa mkutano wa kujadili ukuaji wa miji na athari zake kwa watoto uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya miji Wizara ya Tamisem, Dk Mukuki Hante akifafanua jambo wakati wa mkutano wa kujadili ukuaji wa miji na athari zake kwa watoto uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida.
Baadhi ya washiriki wakichangia maoni wakati wa mkutano wa kujadili ukuaji wa miji na athari zake kwa watoto uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano wa kujadili ukuaji wa miji na athari zake kwa watoto uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya washiriki waliohudhuria mkutano wa kujadili ukuaji wa miji na athari zake kwa watoto uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.


No comments: