Ripoti ya utafiti wa rushwa ya ngono vyuoni wazinduliwa Dar
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Rushwa ya ngono imekuwa ikifanyika katika vyuo vikuu nchini kwa baadhi ya wahadhiri kwa kutumia mamlaka yao kufanya ushawishi wa ngono na baadhi ya wasichana kwa ajili kuwapa viwango visivyoendana na uwezo wao.
Baadhi ya wasichana ambao wamekuwa wamekuwa hawataki kutoa rushwa ya ngono wamekuwa wakipata wakati mugumu katika masomo yao.
Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) kwenye baadhi ya vyuo umebaini kuwepo kwa rushwa ya ngono vyuoni hivyo wadau hawatakiwi kuupuza kwa kupigia kelele na wahusika wanaofanyiwa rushwa hiyo kuvunja ukimya kwa kutoa ushirikiano kwa vyombo vinavyohusika ili kuchukua hatua kwa wahusika kujenga jamii iliyo na maadili.
Hayo yamesemwa na Mwendesha mashitaka wa Takukuru Denis Lekayo wakati akisoma ripoti ya utafiti ikiwa ni maadhimisho ya Siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Amesema utafiti huo umefanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa kushirikiana na Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT) katika vyuo vikuu viwili ambavyo ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) kwa kipindi cha Januari na February mwaka 2019.
Lekayo amesema kufanyika katika vyuo hivyo ni kutokana na historia ya vyuo hivi, umiliki wake (vyuo vya umma) na wingi wa udahili wa wanafunzi na ni vyuo vikuu vikubwa vinavyomilikiwa na serikali.
Lekayo amesema walihojiwa katika utafiti huo ni Watu 589 Kati ya hao UDSM 352 na UDOM 237. Utafiti huu umetumia mbinu ya uchunguzi lengo la kupata taarifa za kina namna rushwa ya ngono kwa wasichana wa vyuo namna inavyotendeka.
Amesema matokeo ya utafiti yanaonyesha wanafunzi waliohojiwa asilimia 81.6 na Watumishi 91.4 walikuwa na uelewa wa dhana ya rushwa ya ngono.
"Kuna mhadhiri mmoja kwa aibu alisema hatamani kuwa sehemu ya taasisi kutokana kuwepo kwa hali hiyo na kudai kuwa katika kupambana kunahitaji kuimarisha mifumo ndani katika vyuo"amesema Lekayo.
Amesema matokeo yanaonyesha zaidi ya asilimia 50 ya waliohojiwa walieleza uwepo wa rushwa ya ngono katika vyuo vikuu vilivyofanyiwa utafiti na kufanya suala hilo kunamaanisha kwamba rushwa ya ngono ni tatizo katika vyuo vikuu hivyo.
Hata hivyo amesema utafiti huo ulitaka kujua sababu zinazochochea rushwa ya ngono katika vyuo vikuu kwa kuwataja wahojiwa kueleza chanzo cha kuwepo vitendo vya rushwa ya ngono.
" Matokeo ya utafiti vyuo vyote viwili yanaonyesha kuwepo kwa sababu tano ambazo ni ukosefu wa maadili, ushawishi wa mtu mwenye mamlaka, mfumo wa utoaji taarifa kutokuwa rafiki, mifumo dhaifu ya kushughulisha rushwa ya ngono na mamlaka ya kutoa alama za mitihani kuachwa kwa wahadhiri pekee." amesema Lekayo
Lekayo amesema katika utafiti huo wamebaini matumizi mabaya madaraka ya kujinufaisha kingono kwa kutoa alama ambazo haziendani na mfanyiwa ngono.
Aidha, amesema kwa upande wa uadilifu mdogo, uongozi na kamati za maadili zinatajwa kutokuwa na maadili na wakati mwingine kamati ya maadili wao wenyewe wanafanya vitu ambavyo vinawafanya watu wasiwaamini na kuna mhadhiri ana ushawishi mkubwa katika kutenda vitendo vya rushwa ya ngono.. mara nyingi malalamiko yanayopelekwa na hayashughulikiwi kutokana mhadhiri kuwa sehemu ya ngono hizo.
Ukosefu wa maadili kwa baadhi ya viongozi na wajumbe wa kamati za maadili kunasababisha kukosekana kwa uwajibikaji Jambo linalosababisha watumishi na wanafunzi kupoteza imani kwa uongozi wa kamati hizo.
Lekayo amesema wahadhiri wapya wanatambua kuwepo kwa muongozo na kanuni za maadili licha ya kudai kutoziona kutokana na upatikanaji wake kutokuwa rahisi.
"Hali hiyo inadhihirika wakati wa utafiti ambao ulikuwa vigumu kupata nyaraka hizi zinazosimamia sera, mifumo na muongozo. Wakati wa utafiti ilibainika nyaraka hizi hupatikana wakati mtumishi ama mhadhiri anapopata matatizo ya kimaadili," amedema Lekayo.
Amesema kitendo cha kuvuja taarifa waathirika wa rushwa ya ngono wengi wamekuwa waoga kutoa taarifa pale wanapobainika au wanapoombwa rushwa hiyo huku vitendo vya rushwa ya ngono vinakiuka kifungo cha 25 cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007 kinachokataza rushwa ya ngono.
Lekayo amesema mtumishi yeyote wa chuo Kikuu mwenye mamlaka ama madaraka anayetumia nafasi yake kumuwekea kigezo cha kupewa ngono mwanafunzi au mtumishi mwenzake anayetaka huduma anakuwa ametenda kosa kwa mujibu wa sheria hiyo.
Aidha, alisema utafiti ulilenga kubaini njia na mbinu zilizotumiwa kufanya ushawishi wa rushwa ya ngono katika tasisi za elimu ya juu.
Amesema matokeo yanaonyesha kuwa mbinu ya utoaji wa alama za chini kwenye mitihani iliongoza kwa kutajwa na wahojiwa ikifuatiwa na vitisho vya kutofaulu kwa wanafunzi.
Lekayo alisema wahadhiri hutumia mwanya huo kwa kuwapa alama ndogo za masomo, kubadilisha alama za ufaulu, kuwafelisha au kuzuia matokeo yao ili kuandaa mazingira ya kuwashawishi kingono huku akidai kuwa kuna mwanafunzi wa Chuo Kikuu Muzumbe amefeli wanafuatilia huku mawasiliano hawayapati.
No comments: