TCRA Saccos yapata mafanikio kwa kuongezeka mtaji


Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

CHAMA Cha Kuweka na Kukopa cha Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ( TCRA-SACCOS)  imefanikiwa katika kuongeza  wa mtaji kufikia sh.bilion 4 mifumo ya Kisasa.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Tisa  wa TCRA Saccos LTD  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Emmanuel Manase amesema kuwa wanachama wa saccos hiyo wamekuwa na ushirikiano na kuweza Saccos kuwa imara.

Dkt. Manase amesema kuwa wanachama waendelee kuwa na ushirikiano ili kuweza kukua na kusaidia kila mmoja kupata kile ambacho alikuwa anategemea.

Nae Mwenyekiti wa TCRA Saccos aliyemaliza muda wake Erasmo Mbilinyi amesema kuwa wamekuwa imara kutokana na viongozi kuweka utaratibu mzuri katika usimamizi.

Mbilinyi amesema wameimarisha mifumo ya Tehama   na kufanya kazi kuwa rahisi na wanachama wanafurahia huduma zinazotolewa na Saccos.

Amesema kuwa moja ya mafanikio wanachama wa Saccos wamekuwa wakiweka hisa na katika gawio kwa mtu Mmoja aliyeweka hisa za juu atapata sh.milioni nane.

Nae Mwenyekiti wa TCRA Saccos  LTD Erasmo Mbilinyi amesema Saccos imekuwa na mafanikio makubwa  ya kuwezesha kukopa kila mwanachama hadi kufikia sh.bilioni 8.5.

Mbilinyi amesema akiba za wanachama zimeongezeka kutoka zaidi ya sh.milioni 99 mwaka 2013 hadi kufikia sh.Bilioni 2 mwaka 2019.

Mbilinyi amesema  madhumuni kuanzisha Saccos hiyo ni kuinua na kustawisha na kuboresha hali ya maisha ya wanachama ili kuweza kukidhi mahitaji mbalimbali ya kijamii na uchumi.


Mwenyekiti wa TCRA Saccos aliyemaliza muda wake Erasmo Mbilinyi akizungumza kuhusiana na masuala mbalimbali ya mafanikio ya Saccos katika kipindi alichoongoza katika mkutano mkuu wa Tisa na Uchaguzi uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja wa TCRA Saccos Damas Mapunda akitoa taarifa mbalimbali za mkutano mkuu  wa Tisa na Uchaguzi  iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Emmanuel Manase akiwa katika picha pamoja na bodi ya TCRA Saccos katika mkutano mkuu wa Tisa na Uchaguzi uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama wa TCRA Saccos wakiwa katika mkutano mkuu wa Tisa na uchaguzi.

No comments: