SERIKALI KUTOA ELIMU YA SHERIA KWA VIONGOZI WA MABARAZA YA ARDHI NGAZI ZA KATA
Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga Amir Mruma akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria ambayo imeadhimishwa kitaifa mkoani Tanga. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na sheria Amon Mpanju akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria ambayo imeadhimishwa kitaifa mkoani Tanga. Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa maadhimisho hayo
Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali
Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga Amir Mruma kulia akifurahia jambo wakati alipofika kutembelea banda la Tawla Mkoa wa Tanga kulia wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio mbalimbaliSehemu ya wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali
Serikali inatarajia kutoa elimu ya sheria kwa viongozi wa mabaraza ya ardhi walioko katika ngazi ya kata ili waweze kutatua migogoro kwa mujibu wa taratibu za kisheria.
Kauli hiyo imetolewa na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga Amir Mruma wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria ambayo imeadhimishwa kitaifa mkoani Tanga.
Alisema Kuwa hapo awali viongozi wa mabaraza hayo yalikuwa hawana elimu ya kisheria katika eneo lao la kazi hivyo walikuwa wanashindwa kuendesha kesi zao kwa sheria na taratibu zilizotungwa na Bunge.
"Kwa utaratibu huu wa sasa uliwekwa na serikali itarahisisha utendaji kazi wa mabaraza hayo lakini hata kesi zinapofika katika ngazi ya Mahakama ,maji wataweza kutuma maamuzi yaliyotolewa katika ngazi ya baraza Kama sehemu ya maelezo ya kesi "alisema Jaji Mruma.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na sheria Amon Mpanju alisema kuwa wiki ya msaada wa kisheria imekuja kwa lengo la kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi wanyonge ambao walikuwa wanashindwa kupata haki zao.
Alisema kuwa wiki hiyo wataitumia kwa ajili ya kuwatembelea wananchi ambao wamefungwa katika maeneo mbalimbali ili kuwasaidia kutoa msaada wa kisheria .
"Kutoa elimu kwa viongozi wa vitongoji na mitaa ili kutatua kero zinazowakabili wananchi kwa kujua sheria husika kusimamia majukumu yao vizutina kupunguza malalamiko na kero zinazowakabili wananchi"alisema Naibu Katibu Mpanju.
Hata hivyo Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela alisema katika mkoa huo zipo kero nyingi ambazo zinazogusa maslahi ya wananchi ikiwemo migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali mkoani hapa.
Alisema kuwa katika jitihada za kutafuta ufumbuzi wa kero ni wamekiwa wakiwashirikisha wanasheria kutoka Chama Cha wanasheria ili kuwasaidia kupata ufunguzi wa migogoro ya ardhi .
"Niwaombe wananchi kutumia wiki hiyo kupata misaada ya kisheria katika kero mbalimbali wanazokabiliana nazo pamoja na kupata elimu ya kisheria ambayo itaweza kuwasaidia kufanya maamuzi mbalimbali"alisema RC Shigela
No comments: