MKUTANO WA 37 WA CHAMA CHA TAA WAFUNGULIWA JIJINI DAR ES SALAAM
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, CPA Aziz Kifile akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa 37 wa Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) Mkutano unaofanyika jijini Dar es Salaam.Wanachama wa TAA na Wakaguzi wa Hesabu za Serikali wakisikiliza mada na hoja zilizowasilishwa katika Mkutano wa 37 wa Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) unaendelea jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu, Ludovick Utouh kulia akisikiliza mada zilizowasilishwa katika Mkutano wa 37 wa Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) unaendelea jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA), CPA Peter Mwambuja akizungumza na Wanachama wa Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) katika ufunguzi wa Mkutano wa 37 wa Chama hicho unaoendelea jijini Dar es Salaam.
Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
CHAMA cha Wahasibu Tanzania (TAA) kimefungua Mkutano wake wa 37, Mkutano unaofanyika siku mbili Novemba 12 na 13, 2020 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam.
Akifungua Mkutano huo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipingo, Mhe. Dotto James, CPA Aziz Kifile amesema Wizara ya Fedha inatambua mchango wa Chama cha Wahasibu katika masuala mbalimbali yakiwemo masuala ya Kodi, kuzingatia misingi ya weledi wa Taaluma zao na kufanya kazi kwa ufanisi.
CPA Kifile amesema, "Katibu Mkuu amewapongeza TAA katika kuhamasisha Wanachama wake katika kujiendeleza Kitaaluma, sambamba na kusimamia misingi ya Taaluma ya Uhasibu ipasavyo na kujikita zaidi katika utoaji wa elimu kuhusu ukusanyaji wa Kodi kwa maslahi ya taifa, hata hivyo amewataka kujihusisha zaidi katika kukuza uchumi wa taifa".
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA), CPA Peter Mwambuja amemuomba Katibu Mkuu Wizara ya Fedha kufukisha ujumbe na salamu za pongezi kwa Mhe Rais kuhusu uongozi wake ambao unawafanya Wahasibu kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya taifa.
CPA Mwambuja amesema Wahasibu wengi wametendea haki nafasi zao katika kuongeza mapato kwa Serikali sambamba na hilo kudhibiti matumizi ya fedha zinazokusanywa, amesema Wahasibu na Wakaguzi wanawajibu kulisaidia Taifa kuhakikisha Rasilimali za taifa na tunu ya mani vinawanufaisha Watanzania wenyewe
Naye Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu, Ludovick Utouh amesema kikao hicho kina maana pia ya kuwakumbusha Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu za Serikali kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa uadilifu wa hali ya juu ili kuchangia maendeleo ya taifa kwa manufaa ya Watanzania wote.
Utouh amesema Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu za Serikali wana wajibu mkubwa kusimamia Usimamizi wa Fedha na Rasiliamli za Taifa ili jitihada za Serikali ya awamu ya tano ziwe endelevu zaidi.
No comments: