MKURUGENZI LONGIDO ATEMBELEA MIGODI INAYOCHIMBWA MADINI YA RUBY WILAYANI LONGIDO,MKOANI ARUSHA
Na Pamela Mollel Michuzi Blog, Longido
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido Dkt Jumma Mhina amefanya ziara ya kutembelea migodi inayochimba madini aina ya ruby inayopatikana Wilayani humo Mkoani Arusha.
Dkt Mhina alitembelea migodi hiyo juzi iliyopo katika eneo la mndarara na kuzungumza na wachimbaji kwa lengo la kuhamasisha,kuelimisha kuhusu ushuru wa huduma sanjari na kuwatia moyo na kusikiliza kero na changamoto wanazopitia Kama wachimbaji
"Hatuwezi tu kuangalia Kodi na ushuru mwingine alafu mfanyabiashara au mchimbaji anadidimia,tunatakiwa kuwapa sapoti na kuhakikisha wanakuwa kiuchumi na kiuchimbaji"alisema Dkt Mhina
Aidha Dkt Mhina aliwapokeza wachimbaji hao kwa kazi kubwa wanaofanya na kuwataka wasikate tamaa kwa kuwa hata Bilionea mpya Sendeu Laizer alipambana na Mungu kamuwezesha kupata madini tani tano yenye thamani ya bilioni 1.7
Alisema kupitia Bilionea huyo mpya Halmashauri yake itapata asilimia 0.0.3 kama ushuru wa huduma sawa na zaidi ya Milioni 5
Aidha aliongeza kuwa Mh Rais John Pombe Magufuli kila siku anaeleza kuwa Tanzania sio nchi masikini na mfano hai ni huo wa Laizer ambapo amepambana na bado ametoa ajira kubwa kwa Vijana wengi
Dkt Mhina aliwatoa hofu wachimba hao na kuhaidi kuwapa ushirikiano mkubwa kupitia serikali yao
Kwa upande wake Bilionea mpya wa Longido Sendeu Laizer alisema kuwa wapo tayari kupokea maagizo yote na kuhaidi kufanyia kazi.Bilionea Laizer alisema soko lake ameshatangaza hadharani kwa mtu yeyote mwenye kuhitaji haijalishi katoka nchi gani yupo tayari kufanya naye Biashara
"Nipo tayari kufanya biashara na mtu yeyote hata kama ni kutoka Marekani au Tanzania"alisema Laizer
Aliweka wazi mipambo yake ikiwa ni pamoja na kuboresha hali ya mgodi ili waweze kuzalisha kwa urahisi pamoja na kuweka miundombinu mizuri
Naye Meneja wa mgodi wa Shedrack Mollel alisema wamefurahishwa na ujio wa Mkurugenzi pamoja na timu yake kwa kitendo cha kuwatia moyo katika shughuli zao za uchimbaji
Mkurugenzi huyo alifanya ziara katika migodi minne inayopatikana eneo la Mundarara
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido Dkt Jumma Mhina akimpongeza Bilionea mpya Sendeu Laizer kwa kupata madini yenye uzito wa tani tano sawa na bilioni1.7
Bilionea mpya Sendeu Laizer akizungumza na vyombo vya habari ambapo alisema yupo tayari kufanya biashara na mtu yeyote mwenye kuhitaji haijalishi katoka nchi gani
Meneja wa mgodi wa Bilionea mpya John Mollel akimueleza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido namna mgodi huo unavyofanya kazi
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido Dkt Jumma Mhina na Bilionea mpya Sendeu Laizer wakiongea na simu kwa njia ya video call watu mbalimbali wakimpongeza
Injinia wa mgodi wa Mndarara ruby mining Benjamin Maige akiongelea namna wanavuofanya shughuli zao za uchimbaji
Injinia wa mgodi wa Mndarara ruby mining Benjamin Maige akimuonyesha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido mahali wanapohifadhi udongo kwaajili ya wananchi
Aliyevalia koti ni meneja mgodi wa Shedrack Mollel,David Ngarioy akizungumza mbele ya Mkurugenzi na timu yake namna wanavyofanya shughuli zao za uchimbaji
No comments: