MHADHIRI MSAIDIZI UDOM AANZISHA USHIRIKIANO WA AINA YAKE...KUWAFIKIA WATU MILIONI 20
MHADHIRI Msaidizi, Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM)ambae ni Mkuu wa taasisi ya Tanzania Community Networks Alliance(tzCNA), Matogoro Jabhera amesema ameamua kuanzisha ushirika wa huduma ya mawasiliano ya gharama nafuu na kusaidia ushirika huo kwenda digitali na mkakati wake ni kuwafikia watu milioni 20 katika kipindi cha miaka mitano.
Ushirika huo ni wa aina yake kuanzishwa nchini Tanzania ambao ni tofauti na ushirika wa fedha yaani SACCOSS tofauti ushirika wa mazao yaani Agriculture and MarketingaCooperative Society( AMCOS) ambao umezoeleka.
Akizungumza kuhusu ushirika huo, Jebhera amesema kwamba lengo lake ni kuwafikishia huduma ya Mtandao watu milioni 20 ndani ya kipindi cha miaka mitano.
Amesisitiza huo ni mwendelezo wa jitihada zake za kutumia teknolojia ya mawimbi ya televisheni yaani "television white space" kwa ajili ya huduma ya mtandao.
Matogoro amesema "Huu ni ushirika maalumu kwa ajili ya vijana na ushirika huu utatoa fursa za ajira kwa vijana wetu na kwa wananchi wote bila kujali viwango vya elimu zao wala fani zao.
Aliendelea kufafanua zaidi na kwamba kwa wale ambao wanahitaji kumfahamu zaidi huduma za mitandao hiyo ya ushirika wanaweza kutembea kwenye tovuti yao inayotambulika kwa barua pepe www.tzcna.or.tz
No comments: