MBUNGE SANGA AWATAKA WACHEZAJI WA TAIFA STARS KUSHINDA DHIDI YA TUNISIA
Charles James na Janeth Rafael, Michuzi TV
MBUNGE wa Makete mkoani Njombe, Festo Sanga amewataka wachezaji wa Timu ya Taifa 'Taifa Stars kuweka uzalendo mbele kwenye mchezo wake dhidi ya Timu ya Taifa ya Tunisia wa kuwania nafasi ya kufuzu kwa michuano ya Mataifa ya Afrika Afcon zitakazofanyika mwaka 2021.
Kikosi cha Taifa Stars kinachonolewa na Kocha Ettiene Ndahiragije kiliweka kambi ya muda mfupi nchini Uturuki kujiandaa na mchezo huo utakaofanyika nchini Tunisia kesho Novemba 13.
Akizungumza na Michuzi Blog, Sanga amesema ana imani kubwa na kikosi hicho kuelekea mchezo huo licha ya kumkosa Nahodha na Staa wake, Mbwana Samatta huku akiwataka watanzania kuiombea dua timu yao ili iweze kufanya vizuri.
Kuhusu ratiba ya michuano ya kimataifa iliyotolewa, Sanga amezitaka timu zitakazowakilisha Nchi kwenye michuano hiyo kuweka mazingira mazuri ya kujiandaa na michezo hiyo kwa kuimarisha vikosi vyao ili viweze kufanya vizuri zaidi kwenye michuano hiyo na kupeperusha Bendera ya Tanzania vema.
" Mimi nimekua kwenye mpira kwa muda mrefu kwa Timu kama Namungo, Simba na Timu za Zanzibar hii michuano tumekua tukirudi nyuma mara kwa mara hivyo niwaombe maandalizi yawe yanafanyika mapema, Simba sina shaka nayo sana ni wazoefu na wamekua wakifanya vizuri mara kwa mara lakini pia tunawaomba wajiandae," Amesema Sanga.
No comments: