MBUNGE SANGA AAHIDI KUSOMESHA VIJANA 10 VETA, MAKETE

 

Mbunge wa Jimbo la Makete, Festo Sanga akipatiwa maelezo ya vifaa vilivyopo katika Chuo cha Veta Makete leo ambapo alialikwa kama mgeni rasmi kwenye mahafali ya Chuo hiko.
Mbunge wa Jimbo la Makete mkoani Njombe, Festo Sanga akizungumza na viongozi, walimu, wazazi na wanafunzi katika mahafali ya Chuo cha Ufundi Stadi VETA Makete leo ambapo alikua mgeni rasmi
Mmoja wa wahitimu wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA Makete akikabidhiwa cheti cha kuhitimu mafunzo yake na Mbunge wa Jimbo hilo Festo Sanga.
Mgeni rasmi katika mahafali ya Chuo cha Ufundi Stadi VETA Makete ambaye ni Mbunge wa Makete, Festo Sanga akisalimiana na wanafunzi wa Chuo hicho wakati alipowasili kwenye mahafali hayo.



MBUNGE wa Jimbo la Makete, Festo Sanga ameahidi kuwasomesha vijana 10 kila mwaka katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA kilichopo Makete.

Akizungumza katika mahafali ya Chuo hicho leo, Sanga amesema ataanza kuwalipia ada vijana 10 wanaotoka kwenye kata mbalimbali za Makete ambao watakua ni wale wenye uhitaji na wanaotoka kwenye mazingira magumu ya kiuchumi.

" Mimi kama Mbunge nitaanza kuwalipia ada vijana 10 tutaandaa utaratibu mzuri wa kuwapata lengo ni kuhakikisha tunakua na Vijana wengi wenye ujuzi na fani mbalimbali ambao hata wakisaidiwa mikopo wana uwezo wa kujiajiri lakini pia kupitia mafunzo watakayopata hapa yatawawezesha kupata ajira sehemu mbalimbali.'' Amesema.

Inasikitisha kuona kati ya wanafunzi 64 wanaohitimu leo wanafunzi wanaotokea hapa Makete hawafiki 10 zaidi ya 50 wanatoka nje hii maana yake tunashindwa kutumia fursa, niwaombe sana ndugu zangu tuitumie fursa ya kupata Chuo hiki ili vijana wetu wafaidikie nayo." Amesema Sanga.

Sanga ameipongeza Serikali kwa kujenga Chuo hicho kikubwa na cha kisasa mkoani Njombe ambacho kina mazingira mazuri na vifaa vya kisasa huku akiahidi kuwa balozi mzuri wa kukitangaza.

No comments: