MAONESHO YA BIDHAA ZA WAJASIRIAMALI YAFANA KATIKA KITUO CHA UTAMADUNI UFARANSA ALLIANCE

 Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KATIKA kuelekea sikuu ya Krismasi na Mwaka mpya Kituo cha Utamaduni cha Ufaransa Alliance kimeamua kuandaa maonesho ya bidhaa mbalimbali za wajasiriamali ikiwa ni sehemu ya kuwawezesha wajasiriamali hao kukutana na wateja wapya.

Kituo hicho ambacho kipo cha Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania umeweka wazi kuwa unaamini kupitia maonesho hayo wajasiriamali hao wakiwemo wale wanaouza bidhaa za mkono ambazo zimetokana na ubunifu wa kitanzania utakwenda kukuza soko la bidhaa hizo kutokana na kukutanishwa na watu kutoka sehemu mbalimbali waliofika kwenye maonesho hayo.

Wakizungumza na Michuzi TV na Michuzi Blog leo Novemba 28,2020 wakati maonesho hayo ya siku moja yaliyoanza saa mbili asubuhi na kuhitimishwa saa moja jioni, baadhi ya wajasiriamali hao wametoa pongezi kwa Kituo cha Utamaduni ya Ufaransa Alliance kwa kuandaa maonesho hayo kwani pamoja na mambo mengine imekuwa fursa kwao kutanua wigo wa kibiashara.

 Akizungumzia maonyesho hayo mjasiliamali Getrude Mtallo kutoka Duka la  Chema Design linalojihusisha na uuzaji wa bidhaa za nguo amesema maonyesho hayo yamewasaidia kuwakutanisha na wateja wapya hasa kipindi hiki cha kuelekea msimu wa sikukuu.

Amesema kuwa katika naonyesho hayo walikuja na bidhaa mbalimbali zikiwemo nguo  mapazia pamoja na bidhaa zingine za mapambo ya ndani, hivyo ametoa shukrani kwa waandaaji wa maonesho hayo.

"Sis tupo hapa hapa jijini Dar es Slaam katika maeneo ya Oyesterbay na kimsingi kwenye maonesha haya tumefanya biashara kidogo japo lakini chakufurahisha tumebadilisha mawasiliano na wateja.Ushauri wangu maonesho haya yawe yanafanyika mara kwa mara na yawe yanatangazwa ili kutoa fursa ya watu wengi kufika,"amesema Getrude.

Kwa upande wake mjasiriamali  Pili Mohamed  amesema maonesho hayo yaliyofanyika kituo cha Utamaduni cha Ufaransa Alliace wanashukuru wamefanya biashara kidogo tofauti na wasingefika kabisa.

 Pili ambaye anafanya shughuli zake za ujasiriamali maeneo ya Sleep Way jijini Dar es Salaam ameweka wazi amefurahi kupata fursa ya kushiriki kwenye maonesho hayo.

Wakati mjasiriamali Salvina Richard amesema baada ya kumalizika kwa maonyesho hayo ya siku moja sasa anarudi kwenye maeneo yake ya biashara ya kila siku yaliyopo Coast Furniture and Hand Craft Masaki huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba Watanzania kutembelea katika biashara zake kuona bidhaa zenye ubora wa hali ya juu.

Awali mwanamziki na mmiliki wa bendi ya bendi ya Seghito Afro Jazz, Aneth Ngongi aliyekuwa akitoa burudani wakati wa maonesho hayo, amesema Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania kupitia kituo hicho cha utamaduni wamekuwa na moyo mkubwa wa kuwasaidia wasanii na wanamuziki wa Tanzania, hivyo nao wanalojukumu la kuendelea kushirikiana nao.

"Pamoja na kuwepo kwa maonesho ya bidhaa mbalimbali, kwetu sisi tumepata fursa ya kutumbuiza watu waliokuwa wanakuja hapa kununua na kuangalia bidhaa zenye ubora.Naamini burudani ambayo tumeitoa itakuwa imewakuna wengi kwani hata sisi tumefurahi kuwepo hapa siku ya leo.Tunafahamu katika kuelekea msimu wa sikukuu kituo kimeona umuhimu wa kuwakutanisha wajasiriamali na wateja wao,"amesema.

Kuhusu bendi yake, amesema tangu imeanzishwa imefikisha miaka nane, na amekuwa akishirikiana a Kituo cha Utamaduni ya Ufaransa Alliance kwa miaka saba sasa na hasa kila wanapopata mualiko huku akitumia nafasi hiyo kutoa rai kwa wananchi kujenga utamaduni wa kutembelea kituo hicho kwani hakuna kiingilio chochote kwa wanaotaka kwenda kushuhudia burudani.

Moja ya wajasirimali akiwa katika eneo lake la biashara wakati wa maonesho ya bidhaa mbalimbali za mikono yaliyofanyika Kituo cha Utamaduni cha Ufaransa Alliance jijini Dar es Salaam.


Mjasiriamali  Pili Mohamed  akipanga bidhaa zake kwenye maonesho ya bidhaa mbalimbali yaliyoandaliwa na Kituo cha Utamaduni cha Ufaransa Alliace.Kituo hicho kimeamua kuandaa maonesho hayo ya siku moja ili kuwakutanisha wajasirimali na wanunuzi katika kipindi hiki cha kuelekea siku kuu ya Krismasi .


Baadhi ya wageni waliohudhuria maonesho ya bidhaa mbalimbali wakiendelea kupata burudani ya muziki kutoka kwa mwanamuziki Aneth Ngongi(hayupo pichani)

Mjasiriamali Salvina Richard akiweka vizuri bidhaa zake za vyungu na vikombe vya udongo baada ya kumalizika kwa maonesho hayo.

Mwanamziki na Mmiliki wa Bendi ya Seghito Afro Jazz, Aneth Ngongi akiwa jukwaani wakati akitoa burudani kwa wageni mbalimbali waliofika kwenye maonesho ya wajasiriamali wadogowadogo yaliyofanyika katika kituo cha utamaduni cha Ufaransa Alliance.

Mwanamziki na Mmiliki wa Bendi ya Seghito Afro Jazz, Aneth Ngongi(kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Masuala ya Utamaduni katika Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania Celile Frobertpo(kushoto) wakiangalia kitu kwenye simu baada ya mwanamuziki huyo kumaliza kutumbuiza.


Wajasiriamali wakiendelea kupanga bidhaa zao baada ya kumalizika kwa maonesho hayo ambayo yamelenga kuwakutanisha wajasiriamali na wateja wao katika kituo hicho cha utamaduni cha Ufaransa Alliance.


Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Masuala ya Utamaduni katika Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania Celile Frobertpo(kulia) akichagua nguo wakati wa maonesho ya bidhaa mbalimbali yaliyofanyika Kituo cha Utamaduni cha Ufaransa Alliance jijini Dar es Salaam.

Getrude Mtallo ambaye ni mfanyabiashara kutoka Duka la  Chema Design linalojihusisha na uuzaji wa bidhaa za nguo akiendelea kupanga nguo zake baada ya kumalizika kwa maonesho hayo yaliyofanyika Kituo cha Utamaduni cha Ufaransa Alliance.

 

No comments: