CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE CHATIMIZA MIAKA 30 KWA MAFANIKIO MAKUBWA

Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa  Ibrahim Juma akizungumza katika hafla ya Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) kutimiza miaka 30 ya utendaji wake toka kilipoanzishwa iliyofanyika kwenye hoteli ya Golden Tulip Masaki jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.

Jaji Profesa Juma amesema TAWLA ni moja ya Taasisi za mwanzo kabisa katika kutoa msaada wa kisheria ,wamekuwa wakitoa msaada kama mawakili lakini pia kama wanasheria, kutoa elimu mbalimbali katika masuala ya kisheria na wamekuwa msaada mkubwa kwa wanawake.

Amesema Mahakama imekuwa ikiwachukulia kama wadau muhimu  sana katika kusaidia wanawake kupata haki na "kama mahakama tumekuwa tukiwapa unafuu maalum mara wanapoleta kesi mbalimbali huwa hawalipii ada na hii inaonesha kuwa mahakama tunawatambua kwa sababu tunajua wanatoa msaada hasa kwa wanawake ambao wengi wao wamekuwa wakinyimwa haki zao".

Ameongeza kuwa katika nchi yetu na nchi zingine  unapozungumzia watu ambao hawana nafasi sana katika masuala ya kisheria, Kiuchumi na mengine mengi ni wanawake hata umoja wa mataifa wanajua hilo  kwa sababu wengi wao wako vijijini ambako hakuna mahakama

Sasa ili kupata haki zao inabidi watembee mwendo mrefu kufuata haki katika mahakama hivyo taasisi kama TAWLA huwa zinawafuata waliko zinawaelimisha masuala ya kisheria, kuwasikiliza shida zao na kuwapa msaada wa kisheria jambo ambalo limesaidia sana wanawake kupata haki nchini.

Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha wanasheria wanawake (TAWLA) Bi. Lulu Ng’wanakilala akizungumza wakati hafla ya chama hicho kutimiza miaka 30 ya utendaji kazi wake tangu kilipoanzishwa hapa nchini iliyofanyika kwenye hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA)Tike Mwambipile  akimkaribisha Makamu mwenyekiti wa Chama hicho ili kumkaribisha mgeni rasmi Jaji Profesa Ibrahimu Juma ili kuzungumza na wanachama.

Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa  Ibrahim Juma akizindua kitabu chapisho la Chama cha Wanasheria Wanawake TAWLA katika hafla ya chama hicho kutimiza miaka 30 ya utendaji wake tangu kuanzishwa kwake,iliyofanyika kwenye hoteli ya Golden Tulip Masaki jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.Katikati ni Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha wanasheria wanawake (TAWLA) Bi. Lulu Ng’wanakilala na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA) Tike Mwambipile .

Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa  Ibrahim Juma kwa pamoja na  Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha wanasheria wanawake (TAWLA) Bi. Lulu Ng’wanakilala na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA)Tike Mwambipile  wakionesha machapisho hayo mara baada ya kuzinduliwa.

Jaji Mkuu wa Tanzania  Profesa  Ibrahim Juma akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA) Tike Mwambipile katika hafla hiyo iliyotolewa na chama hicho kwake kutambua mchango wake katika utendaji kazi katikati ni Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha wanasheria wanawake (TAWLA) Bi. Lulu Ng’wanakilala.

Jaji Mkuu wa Tanzania Jaji Profesa  Ibrahim Juma,  Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA) Tike Mwambipile, Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha wanasheria wanawake (TAWLA) Bi. Lulu Ng’wanakilala pamoja na wanachama wengine wa chama hicho wakikata keki katika hafla hiyo.

Picha mbalimbali zikionesha baadhi ya wanachama wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania TAWLA walioshiriki katika hafla ya kutimiza miaka 30 tangu kuanzishwa kwa chama hicho hapa nchini.

Jaji Winfrida Koroso Mwanachama mwandamizi wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania TAWLA kushoto akishiriki katika hafla hiyo pamoja na wanachama wenzake.

Jaji Mkuu wa Tanzania Jaji Profesa  Ibrahim Juma,kulia Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha wanasheria wanawake (TAWLA) Bi. Lulu Ng’wanakilala katikati na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA) Tike Mwambipile wakifurahia jambo katika hafla hiyo.

Mwanamuziki Aneth Kushaba akitumbuiza katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA) Tike Mwambipile pamoja na wanachama wenzake wakisakata Kwaito katika hafla hiyo.

No comments: