ADEN MOHAMMED ACHAGULIWA KUONGOZA CHAMA CHA SOKA MKOA WA DODOMA

 


WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Soka Mkoa wa Dodoma(Dorefa) wamechagua aliyekuwa Mwakilishi wa Klabu Kanda ya Dodoma Singida,Aden Mohammed kuwa Mwenyekiti mpya wa Chama Cha Soka Mkoa  Dodoma  (Dorefa.)

Akitangaza matokeo leo Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili msomi, Benjamin Karume alimtangaza Aden kuwa mshindi wa nafasi hiyo  kwa kupata kura 21 baada ya kumbwaga Kaimu Mwenyekiti wa Chama Makocha (TAFCA) Taifa Lister Manyara aliyeambulia kura moja.

Akizungumza Mara baada ya kuchaguliwa Aden aliahidi kuchapa kazi huku akiomba ushirikiano.

Katika nafasi ya Katibu Mkuu,Wakili Msomi Karume amemtangaza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho kurudi tena katika nafasi hiyo,Hamisi Kissoy.

Kissoy alipata kura 20 huku Charles Komba akiambulia kura 1 kati ya kura 22.

Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti,Karume amemtangaza,Nsekela Masanilo kushika nafasi hiyo Mara baada ya kupata kura 22,Masanilo alikuwa Mgombea pekee katika nafasi hiyo.

Karume pia amemtangaza Mweri Hamsini kuwa Katibu Msaidizi wa Dorefa ambaye amepata kura 22.Mweri alikuwa Mgombea pekee.

Katika nafasi ya Mwakilishi wa Klabu Mwanasheria Maurice Sarara ameibuka na ushindi kwa kupata kura 22.Sarara alikuwa Mgombea pekee katika nafasi hiyo.

Katika nafasi ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu TFF,Dickson Kimaro ameibuka na ushindi kwa kupata  kura 21 huku Khalifa Ibrahim maarufu kwa jina la P.DIDDY  Akipata kura 1

Katika nafasi ya Wajumbe wa Kamati Tendaji

Willbert Sihaba 20

David Sekimanga 21

Judith Myeya 6

Dominick Albinius 2

Washindi ni Sihaba na Sekimanga ambapo Karume ameitaka Kamati ya Utendaji ya Dorefa iitishe uchaguzi mdogo kujaza nafasi moja ambayo haikupata mshindi kutokana na kanuni kutaka mshindi kufikisha nusu ya kura zilizopigwa.

No comments: