Waziri Hasunga aongoza uzinduzi wa muongozo wa uzalishaji wa zao la Mpunga


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Waziri wa kilimo nchini Tanzania Japhet Hasunga ameongoza zoezi la uzinduzi mpango jumuifu yenye lengo la kuwaelimisha wataalamu na wananchi jinsi ya kuzalisha,kuhifadhi na kutumia mazao mbali mbali ili kuboresha lishe na kipato katika ngazi ya kaya na kitaifa.

Serikali imezindua miongozo ya kanuni na tekinolojia bora ya uzalishaji na usimamizi wa mazao ya Pili pili hoho,mboga za majani,Bamia,Nyanya,Karoti,
Kabichi,Vitunguu na usimamizi wa mazao yote ya mboga mboga na Matunda.

Uzinduzi huo umefanyika mkoani Njombe kabla ya kuhitimisha kilele cha siku ya chakula Duniani ambayo kitaifa imefanyika mkoani Njombe katika halmashauri ya mji wa Njombe.

Lakini vile vile serikali imezindua muogozo wa kufundisha uzalishaji na usimamizi wa zao la mpunga kwa ajili ya matumizi mbali mbali.

Aidha waziri Hasunga ametumia fursa hiyo kuwaomba wadau kutumia miongozo hiyo kuwaelimisha wananchi ili kuhakikisha wanakabiliana na changamoto kwenye kilimo  


No comments: