Waziri Hasunga ahitimisha kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani mkoani Njombe
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa ameshika samaki aina ya Jodari akimuonesha mgeni rasmi, Waziri wa Kilimo mhe. Japheth Hasunga wakati wakitembelea mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maadhimisho ya siku chakula duniani inayoadhimishwa kitaifa mkoani Njombe leo Oktoba 16,2020.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo)Prof. Elisante Ole Gabriel akitoa taarifa ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi leo (16.10.2020) kwenye Kilele cha Maadhimisho ya 8 ya kitaifa ya Siku ya Chakula duniani kilichofanyika kwenye viwanja vya Mji mwema Mkoani Njombe.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo)Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea cheti cha pongezi kwa Wizara yake kushiriki Maadhimisho ya 8 ya kitaifa ya Siku ya Chakula Duniani kutoka kwa Mgeni rasmi wa Kilele cha Maadhimisho hayo ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga leo (16.10.2020) Mkoani Njombe. Meneja wa Shamba la Mifugo la Kitulo Bw. Gerald Mashurano (kushoto) akifafanua jambo kwa Mgeni rasmi wa Kilele cha Maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Chakula Duniani Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kutoka kushoto) baada ya Mhe. Hasunga kufika kwenye banda la shamba hilo leo (16.10.2020) Mkoani Njombe. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel .
No comments: