SERIKALI YAZITAKA TAASISI KUBWA ZA FEDHA KUVISAIDIA VYAMA VYA USHIRIKA KUWEKA NA KUKOPA

 
Na Woinde Shizza , Michuzi Tv Arusha

Naibu katibu mkuu wa wizara ya kilimo profesa Siza Tumbo amezitaka taasisi za fedha zilizofanikiwa kuvisaidia vyama vya akiba na mikopo kuondokana na matatizo yanayokwamisha ustawi wake likiwemo la kuandamwa na migogoro.

Prof Tumbo aliyasema hayo leo jijini hapa alipokuwa akifunga maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vyama vya ushirika wa akiba na mikopo duniani  ambapo alisema ni vyema viongozi wa ushirika wakakaa na kuangalia namna watakavyoondoa migogoro hiyo ili vyama hivyo viendelee kukuwa.
 
Kwa upande wa Meneja Biashara wa Benki ya CRDB,Kanda ya Kaskazini,David Peter alisema kuwa Benki yao imekuwa ikishirikiana Sana na vyama vya ushirika wa akiba na mikopo na hadi sasa wamesha shirikiana na vyama vya ushirika zaidi ya 450 ,pia wameshatoa mikopo ya zaidi ya bilioni 300 kwa vyama hivyo.

Aidha alisema kuwa wamekuwa wakichangia kusaidia vyama hivi , wamekuwa wanashiriki kuwajengea uwezo wa vyama kuanzia kwa watendaji na bodi zake ,katika vipindi tofauti tofauti wamekuwa wakitoa mafunzo nchi nzima kwa vyama vyote vya ushirika ambavyo vimeingia ubia na Benki ya CRDB ,Kuhakikisha wanakuwa na uwezo sahihi na uelewa katika kusimamia shughuli za kifedha Ndani ya vyama vyao vya Sacco's.

"Hii imewezesha vyama kuwa endelevu na pia imewezesha kutunza fedha zao vizuri na pia kutoa mikopo na kuwezesha wananchi wale ambao wanapewa mikopo wanarejesha kwa wakati  na tunaendelea kuona vyama hivi vinaendelea kukuwa "alisema David

Aliwaasa wananchi wasiweke pesa Ndani ambapo apana usalama Bali wapeleke pesa Benki ,pia waweke Ela sehemu ambayo wanapata faida nawaache kuweka fedha sehemu ambazo awapati faida .

Kwa upande wa migogoro alisema kuwa Ni vyema vyama  wakakaa na kuangalia namna ya kutatua migogoro waliyonayo , waangalie ni sehemu gani wanakosea wakajirekebisha,pia Ni vyema wakatafuta Benki Kama CRDB ikawajengea viongozi uwezo wa kutambua Mambo mbalimbali Kama kujua namna soko la fedha linavyoenda Baadhi ya wataalam wa maswala ya fedha wamesema tatizo kubwa linalovikabili vyama vingi vya ushirika wa akiba na mikopo Ni pamoja na kufanya biashara kwa mazoea na kutafuta njia za mkato.

Mtaalam wa maswala ya fedha  Prof Alfred Sife alisema tatizo la kutofuata Sheria Ni kubwa pia Asilimia kubwa ambapo hivi karibuni vyama zaidi ya elfu Tatu (3000)vimefutwa

No comments: