MRADI WA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO KIPINDI CHA CORONA WAFUNGWA SHINYANGA Inbox
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Hoja Mahiba akizungumza wakati wa kikao cha kufunga Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Hoja Mahiba amewataka wadau wa haki za wanawake na watoto kuunganisha nguvu pamoja katika kukabiliana na matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwani bado yanaendelea kujitokeza katika halmashauri hiyo.
Mahiba ametoa rai hiyo leo Alhamis Oktoba 15,2020 wakati wa kikao cha kufunga Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’ uliokuwa unatekelezwa katika kata 10 za halmashauri ya Shinyanga.
Mradi huo ulilenga kuongeza uelewa wa madhara ya Ugonjwa wa Corona katika kulinda haki za wanawake na watoto uliokuwa unatekelezwa na halmashauri hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Thubutu Africa Initiatives, Rafiki SDO na ICS kwa ufadhili wa Shirika lisilo la kiserikali la Women Fund Tanzania (WFT).
Mahiba alisema suala la ukatili wa kijinsia ni mtambuka hivyo ni jukumu la kila mmoja katika jamii kushiriki katika mapambano ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
“Matukio ya ukatili bado yanaendelea kujitokeza katika jamii, wanawake wanauawa,wanabakwa na watoto wanakatishwa masomo yao. Kila mmoja asimame kwa nafasi yake kumkomboa mwanamke na mtoto. Na katika vita hii asiachwe mtu nyuma, wanaume,wanawake na watoto washirikishwe ili kukabiliana na vitendo vya ukatili”,alisema Mahiba.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Muhoja aliwatupia lawama baadhi ya askari polisi katika kituo cha Didia akidai kuwa wamekuwa wakivujisha siri /taarifa za wasamaria wema wakiwemo wahanga wanaotoa taarifa za matukio ya ukatili hivyo kuliomba jeshi la polisi kuangalia namna ya kutatua changamoto hiyo.
“Katika kutekeleza mradi huu pia tumekumbana na changamoto ya baadhi ya Maafisa Watendaji wa kata ambao nao wanavujisha taarifa za wasamaria wema wanaotoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia. Lakini pia bado kuna changamoto ya unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu”,alisema Muhoja.
“Wakuu wa Idara, maafisa elimu msingi kaeni na walimu wenu muwaeleze kuacha kutelekeza familia,watunze familia zao, Afisa Utumishi waambie watendaji wa kata na vijiji kwani miongoni mwao wanatajwa kutelekeza familia na baadhi ya maafisa maendeleo ya jamii wa kiume nao wametajwa kutelekeza familia”,aliongeza Muhoja.
Mkurugenzi huyo wa halmashauri alitumia fursa hiyo kulishukuru shirika la WFT kuwawezesha ruzuku kutekeleza mradi huo kuongeza ufahamu na uelewa wa madhara ya Corona katika kulinda haki za wanawake na watoto katika kata za Bukene, Didia, Mwantini, Iselamagazi, Pangagichiza, Mwakitolyo, Salawe, Lyabukande, Lyabusalu na Solwa.
Nao wadau walioshiriki katika kutekeleza mradi huo walieleza kuwepo na hofu kwa baadhi ya watendaji wa kata wanaposhughulikia kesi za ukatili wa kijinsia wanaogopa kuwa mstari wa mbele kupeleka kesi kwenye vyombo vya dola.
“Jamii ina uoga wa kutoa taarifa za watu wanaofanya ukatili. Wananchi waliotendewa ukatili nao hawatoi taarifa wanaona ni kama ni sehemu ya maisha yao”,alisema Mratibu wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’ kutoka Shirika la Rafiki SDO, George Nyanda.
Meneja Miradi kutoka Thubutu Africa Initiatives ,Paschalia Mbugani alisema Bado kuna changamoto ya ajira kwa watoto mgodi wa Mwakitolyo na kwamba Jeshi la jadi sungusungu limekuwa likitumia nguvu kubwa na kuchangia vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Meneja Miradi wa Shirika la ICS ,Sabrina Majikata alisema hivi sasa kuna ongezeko la utoaji taarifa za matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto lakini pia sasa wanaume wameanza kushiriki katika malezi ya watoto.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Edmund Ardon alisema changamoto waliyokutana nayo ni utekelezaji wa familia unaofanywa na watumishi wa umma kama walimu na watendaji na wengine katika jamii huku akidokeza kuwa kumezuka tabia ya wazazi na walezi kuozesha watoto nyakati za usiku.
Naye Mkurugenzi wa shirika la AGAPE ACP, John Myola aliipongeza halmashauri kuwa wakweli mfano kuweka wazi suala la baadhi ya watumishi wa umma kutelekeza watoto na kuwaomba wadau kuendelea kushirikiana ili kumaliza matukio ya ukatili wa kijinsia.
“Changamoto za ndoa za utotoni zimeanza kuisha kwani sasa jamii ina uoga ndiyo maana hata ndoa za utotoni zimekuwa zikifanyika usiku kutokana na uoga kuwa hilo siyo jambo jema.Tatizo ni baadhi ya viongozi kwenye kata na vijiji hawataki lawama kuhusu kesi za ukatili dhidi ya wanawake na watoto”,alisema Myola.
Kikao cha kwanza kutambulisha mradi kilifanyika Juni 30,2020 kutambulisha watekelezaji wa mradi huo wa miezi mitatu ambao ni Rafiki SDO, Thubutu Africa Initiatives na ICS wa ufadhili wa Shirika la WFT na leo kikao cha kufunga mradi huo kililenga kuangalia malengo na mafanikio yaliyofikiwa wakati wa kutekeleza mradi huo kwa kipindi cha miezi mitatu, (Juni – Septemba) changamoto zilizojitokeza na kuweka mikakati endelevu ya utekelezaji wa kulinda haki za wanawake na watoto.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Hoja Mahiba akizungumza leo Alhamis Oktoba 15,2020 katika ukumbi wa Hospitali ya wilaya ya Shinyanga wakati wa kikao cha kufunga Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’ uliokuwa unatekelezwa na halmashauri ya Shinyanga na mashirika ya ICS, Rafiki SDO na Thubutu Africa Initiatives. Kulia ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Dk. Mameritha Basike, kushoto ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Muhoja. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Hoja Mahiba akiwasihi wadau wa haki za wanawake na watoto kuungana pamoja katika mapambano ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Hoja Mahiba akilishukuru Shirika la WFT kwa kufadhili Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Muhoja akizungumza wakati wa kufunga Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Muhoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Mhe. Hoja Mahiba (kulia) wakiwa ukumbini.
Meneja Miradi wa Shirika la ICS ,Sabrina Majikata akielezea namna walivyotekeleza mradi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’.
Meneja Miradi kutoka Shirika la Thubutu Africa Initiatives ,Paschalia Mbugani akielezea namna wanavyoshiriki katika mapambano ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Mratibu wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’ kutoka Shirika la Rafiki SDO, George Nyanda akielezea namna walivyotekeleza mradi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Edmund Ardon akielezea namna walivyotekeleza namna walivyotekeleza mradi wa Mradi wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Kipindi cha Mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ‘COVID - 19’.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini
Afisa wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia na Watoto, Vivian Zabron akieleza namna jeshi la polisi linashiriki katika mapambano ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Mwanasheria wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Salehe Hassan akitoa ufafanuzi wa kisheria kuhusu masuala ya kulinda haki za wanawake na watoto.
Mkurugenzi wa Shirika la AGAPE ACP, John Myola akiipongeza halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa kuendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika mapambano ya ukatili wa kijinsia.
Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Samuye Ibrahim Bundo akichangia hoja ukumbini.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Dk. Mameritha Basike akizungumza ukumbini na kuomba jeshi la polisi kushughulikia haraka kesi zenye ushahidi wanazowapatia kuhusu matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Mjumbe wa kamati ya usimamizi wa mradi kutoka WFT, Irene Laulent kutoka kata ya Usanda katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga akichangia hoja ukumbini namna ya kukabiliana na matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini
No comments: