RC KIMANTA:UMEFIKA WAKATI MUAFAKA KUUNGANISHA NGUVU ZA PAMOJA KUANGAMIZA GUGU KAROTI

Mkuu wa mkoa wa Arusha Iddy Kimanta akibadikishana mawazo na Mwenyekiti wa kamati ya gugu karoti mkoa wa Arusha Ndelekwa Kaaya.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Iddy Kimanta akiwa pamoja na wakuu wa Wilaya ya Arusha mjini,Monduli,Arumeru,Karatu 
Mkuu wa mkoa wa Arusha Iddy Kimanta na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Edward Balele akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa kupambana na gugu karoti mkoani Arusha katika maadhimisho ya siku ya gugu Karoti Mkoa wa Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Iddy Kimanta pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Edward Balele akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya kutokomeza gugu karoti mkoa wa Arusha.
Mtafiti wa visimbufu na viwatilifu vya mimea TPRI Maneno Chidege akiwasilisha mada na kujibu maswali ya wadau mbalimbali walioshiriki katika maadhimisho ya siku ya gugu karoti mkoani Arusha 
Baadhi ya washiriki wa Maadhimisho ya siku ya gugu karoti mkoa wa Arusha Wakiwemo wakulima kutoka sehemu mbalimbali mkoa wa Arusha 
Baadhi ya washiriki wa Maadhimisho ya siku ya gugu karoti mkoa wa Arusha zikiwemo taasisi mbalimbali za kilimo na utafiti na Mazingira  kutoka sehemu mbalimbali mkoa wa Arusha


Na.Vero Ignatus ,Arusha

Serikali imesema umefika wakati muafaka wa kuunganisha nia ,maarifa na nguvu katika kuangamiza gugu karoti kwani inatambua madhara ambayo  yamekuwa na athari katika  uchumi na jamii kwa ujumla

Akizungumza katika maadhimisho ya tano ya gugu karoti mkuu wa mkoa wa Arusha Iddy Kiman'ta serikali inatambua na imekuwa ikichukua hatua kadhaa katika kuelimisha wananchi, utafitiwa kisayansi ,kutafuta njia sahihi na rafiki wa mazingira ya kutokomeza gugu, bila kuathiri na kuharibu mazingira.

Alitoa rai kwa wadau wote kuwa ni vyema taasisis zote kushirikiana katika kutokomeza gugu karoti kwa kutumia njia rafiki kwa mazingira ,amezitaka taasisi zishirikiane na zifanye kazi kwa karibu na halamashauri hususani vijana na wanawake sambamba na kutafuta fedha kutoka kwa wadau wa maendeleo ili juhudi hizi ziwe endelevu.

Akisoma risala ya kwa niaba ya kamati ya gugu karoti mkoani Arusha Anna Sirikwa alisema ukubwa watatizo la kusambaa kwa gugu karoti mkoani umekuwa na kasi ya kutisha,wanajamii kutokuchukua hatua kwa kutokujua ukubwa wa athari athari zitokanazo na gugu hilo

Kamati kutokuwa na uwezo wa kwenda maeneo ya mbali kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha jamii kuhusiana na gugu hilo kwa mapana zaidi,sambamba na kamati hiyo kutokuwa na ofisi kwaajili ya kuratibu shughuli za gugu karoti za kila siku.

Aidha walito pendekezo kwamba wanaiomba serikali ngazi ya mkoa iingilie kati suala la kupambana na gugu karoti kama inavyoingilia suala la kuteketeza mifuko ya plastiki na usafi wa maeneo kila wiki ya mwisho wa mwezi.

Pia wamemuomba mkuu wa mkoa kuwaunganisha na mkuu wa magereza ili kamati iweze kwenda kutoa elimu kwa wafungwa waweze kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo pamoja na TANROAD Kwaajili ya kutoa elimu kwa wafanyakazi wao na mawakala wanaohusika kufanya usafi pembezoni mwa barabara .

Amesema kuwa siku hii ya leo inamalengo ya kuielimisha na kuhamasisha jamii,walifahamu na kulijua gugu karoti ili waweze kuchukua harua stahiki za kuliangamiza ili kuzuia madhara .

Kiman'ta  amesema ni kutoa fursa kwa mashirika ,makampuni na wananchi ili wawe mstari wa mbele katika kuangamiza sio tu kuangamiza gugu karoti lakini pia magugu mengine hatarisi yaliyopo nchini Tanzania .

Ni dhahiri katika mapambano yanamuhusu kila mwananchi awe mdau wa vita dhidi ya gugu karoti ili tuweze kufanikiwa lazima kushikamana kwa pamoja ili kulitokomeza

Elimu hii inatakiwa iwe ni peogram ya kitaifa ili viongozi wote wafahamu na kutafuta namna ya kulitokomeza,waliwemo wanafunzi,wananchi ,taasisi za kilimo,watafiti na wadau mbalimbali katika kulidhibiti gugu hilo

 Jitihada za kutokomeza gugu karoti mkoani Arusha ilianza rasmi 2016 katika mji mdogo wa ngaramtoni wilaya ya Arumeru,gugu hilo lenye uwezo wa kuzaa mbegu 30,000 kwa mzao mmoja ambapo linauwezo wa kuzaa mara 3 kwa mwaka . 

Mwisho

No comments: