PROF.SHEMDOE AONGOZA KIKAO KAZI KUJADILI MAPITIO YA SERA YA VIWANDA VIDOGO NA VYA KATI

 

Katibu Mkuu Prof. Riziki Shemdoe akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya wizara mara baada ya ufunguzi wa kikao kazi cha mapitio ya sera ya Viwanda vidogo na biashara ndogo .

Katibu Mkuu Prof. Riziki Shemdoe (Aliyesimama) akizungumza wakati wa kikao kazi cha Menejimenti ya wizara cha mapitio ya sera ya Viwanda vidogo na biashara ndogo,  kushoto kwa Katibu Mkuu ni Naibu Katibu Mkuu Ludovick Nduhiye, na kulia kwa Katibu Mkuu ni Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Prof. Raphael Chibunda.

Baadhi ya wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na wadau mbalimbali waliohudhuria kikao kazi cha mapitio ya sera ya Viwanda vidogo na biashara ndogo

……………………………………………………………………………..

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe, leo ameiongoza menejimenti ya wizara katika kikao kazi cha kujadili mapitio (Background paper) ya sera ya viwanda vidogo na vya kati ya mwaka 2003.

Katika kikao hicho kilichohudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu ndugu Ludovick Nduhiye, wakuu wa Idara na Vitengo kutoka wizara ya viwanda na biashara, wawakilishi kutoka sekta binafsi (TPSF),  Taasisi mbalimbali za serikali  pamoja na wadau wa maendeleo nchini ambao ni Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT).

Prof. Shemdoe amesema kwamba wizara imedhamiria kutunga sera za kuwawezesha wajasirimali wadogo kuendeleza biashara ambapo katika blue print tozo mbalimbali ziliondolewa kwa lengo la kuboresha mazingira bora ya wafanyabiashara. Hivyo katika sera hii itawezesha wajasiliamali kufanya shughuli zao kwa urahisi pia uhakika wa mitaji na mikopo.

Naye Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Prof. Raphael Chibunda ameipongeza wizara kwa maamuzi ya kuchagua eneo la SUA kwa ajili ya kikao kazi hicho pia amesema shughuli za kilimo zinaenda sawia na uendelezaji wa viwanda ambayo ndio ajenda ya nchi hii, hivyo basi ili viwanda vizalishe bidhaa za kutosha ni lazima malighafi za kilimo ziwe za kutosha kukidhi viwanda vyetu, Prof. Chibunda alisema pia sera hiyo itasaidia wakulima wanaojishughulisha na uzalishaji wa mazao ya kilimo kuwezeshwa katika mitaji na mikopo nafuu kuendeleza shughuli zao.

Mapitio ya sera ya viwanda vidogo na biashara ndogo yaliwasilishwa na mtaalamu mwelekezi ambaye ni Dkt. Josephat Kweka na kupokea maoni ya kuboresha maeneo mbalimbali kutoka kwa menejimenti ya wizara na wadau waliohudhuria kikao kazi hiki.

No comments: