NMB YATOA MSAADA KWA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA IRINGA
Meneja wa Benki NMB tawi la Ruaha manispaa ya Iringa, Focus Lubende
akizungumza na wafanyakazi wa benki ya NMB ikiwa moja ya kuboresha huduma kwa wateja katika wiki ya huduma kwa mteja wa benki hiyo. Wanyakazi wa benki ya NMB wakiomba dua kabla ya kuanza kikao cha pamoja kuhusu huduma kwa kwa wateja. Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya NMB, wakimkabidhi zawadi ya begi mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Wilolesi Wanyakazi wa benki ya NMb wakiwa pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Mapinduzi mara baada ya kuwatembelea na kuwapa zawadi mbalimbali.
Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa NMB Plc Nchini ,Abella Tarimo
(mwenye rasta) akikabidhi moja msaada wa vitu mbalimbali kwa mganga mkuu wa hospitali ya rufaa (kushoto) Dk. Robert Salim na Mganga Mfawidhi Dk. Alfred Mwakalebela (kulia) Dk. Robert Salim akiongea na wafanyakazi wa benki ya NMB kuwashukuru kwa msaada wa vifaa mbalimbali walivyokabidhi hospitalini hapo vyenye thamani ya sh milioni 4. Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa NMB Plc Nchini ,Abella Tarimo
akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa kwa uongozi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Iringa Hassan Msuna mmoja wa wafanyakazi wa benki ya NMB akitoa elimu kwa
wanafunzi wa saint Dominic juu ya elimu ya kuwa na mipango na kuhifadhi
fedha benki kuhudu huduma mpya ya tatu za kibabe zinazotolewa na benki ya NMB
***************************************
NA DENIS MLOWE,IRINGA
KATIKA kuadhimisha wiki ya huduma kwa Mteja Benki ya NMB imetoa msaada wa
vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh. milioni nne katika Hospitali ya Rufaa
mkoani Iringa na zawadi za vifaa vya shule kwa wanafunzi wa shule tatu za
msingi zilizoko katika manispaa ya Iringa.
Vifaa mbalimbali vilivyotolewa na benki ya NMB kwa hospitali ya rufaa ya
Iringa inayokabiliwa na changamoto mbalimbali ni mashuka, vifaa vya
kujifungulia kwa akina mama, na vitu mbalimbali kwa ajili ya watoto ambavyo
vimekabidhiwa na Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa NMB Plc Nchini
,Abella Tarimo mbele ya mganga mkuu wa hospitali hiyo Dk. Robert Salim
mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dk. Alfred Mwakalebela.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Abela Tarimo alisema Benki ya
NMB imejiwekea utaratibu maalum wa kurejesha kwa jamii asilimia moja ya
faida wanayoipata ikiwa ni sehemu ya shukrani kwa wadau wa benki hiyo
nchini hasa katika sekta za elimu, afya na jamii kwa ujumla.
Tarimo alisema kuwa msaada huo umekuja wakati benki hiyo iko katika wiki ya
huduma kwa wateja na kuweza kuwakutanisha wafanyakazi wa benki ya NMB
kutoka kanda ya Ziwa, kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Dar es
Salaam waliokutana mkoani Iringa kwa ajili ya maadhimisho hayo.
Alisema kuwa benki ya NMB ina wadau na ni sehemu ya jamii hivyo ina una
utaratibu wa watoa huduma kupata nafasi ya kwenda kurudisha fadhila na
shukrani kwa jamii inayowazunguka kwa kutambua kwamba jamii na baadhi ya
sekta zinakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo kama NMB ina uwezo wa
kuzitatua.
“Tunatambua kwamba baadhi ya sekta zinakabiliwa na changamoto ikiwemo sekta
ya afya hivyo kama NMB inatambua kwamba kuna kina mama wanajifungua na
hawana vifaa vya kujifungulia hivyo nafasi hii tumetumia kuleta vifaa hivyo
kwa hospitali ya rufaa ya Iringa” alisema
Alisema kuwa licha ya mashuka pia wamekabidhi hospitali hapo, pampasi za
watoto, mafuta ya kujipaka, sabuni, rubber shit zinazotumika kwa ajili ya
kuweka chini ya mashuka kwa kina mama wakati wa kujifungua.
Aliongeza kuwa watoa huduma wa Benki ya NMB wakati wote wanaamini katika
kugusa na kubadili maisha ya wanajamii, ushiriki wa Wafanyakazi katika
programu za kuisaidia jamii umeongezeka maradufu ukichangiwa zaidi na ari
waliyonayo kutaka kupunguza changamoto na kero zilizopo kwenye jamii
inayowazunguka na wanayoihudumia.
Aidha Mganga mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk. Robert Salim ameishukuru Benki ya
NMB kwa msaada huo akieleza kuwa umefika wakati muafaka kwani kumekuwa
upungufu wa baadhi ya vifaa kulingana na idadi ya wagonjwa wanaohudumiwa
hospitalini hapo kutoka ndani na nje ya mkoa.
Dk. Salim alisema kuwa hospitali hiyo inategemewa na mkoa mzima na mkoa wa
jirani hivyo upungufu wa vifaa hivyo upo kwani wagonjwa ni wengi lakini
kuna upungufu wa vitanda, mashuka na vitendea kazi hivyo kitendo cha NMB
kuleta baadhi ya vifaa hivyo imefanikiwa kutatua changamoto hizo.
Dk Salim alitoa rai kwa uongozi wa kwa benki ya NMB na wafanyakazi hao wa
kuendelea kushirikiana na hospitali ya rufaa ya Iringa na sekta nyingine
katika kutatua changamoto zinazowakabili kwani NMB imekuwa rafiki na jamii
katika kusaidia changamoto mbalimbali nchini.
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali hiyo dk. Alfred Mwakalebela
alisema kuwa hospitali hiyo ina vitanda 377 na kwa wastani wanakuwa na
wagonjwa 300 hadi 400 na wanatumia mashuka 600 hivyo wagonjwa wakikaa kwa
muda wa siku tatu wanatumia mashuka 1800 hivyo kitendo cha NMB kuleta
mashuka kitasaidia sana.
Alisema kuwa msaada huo kwa wodi ya wazazi umelenga sehemu sahihi kwani
yatasaidia sana kwa kina mama katika kuwapatia huduma na kuwasaidia watoto
kutokana na msaada wa pampasi zililetwa hospitalini hapo.
Licha ya msaada wa Benki ya Nmb kwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa,
wafanyakazi wa benki hiyo walitoa zawadi mbalimbali kwa shule tatu za
msingi zilizoko manispaa ya Iringa ikiwemo mipira, vifaa vya shule kama
rula, pen na penseli, tisheri, kofia, vibubu na kuwapa elimu ya uhifadhi wa
fedha kwa wanafunzi hao kuhusu akaunti za watoto zinazotolewa na benki hiyo.
Shule zilizotembelewa na benki hiyo ni shule ya msingi Mapinduzi, shule ya
msingi Wilolesi na shule ya Msinga Saint Dominic ambapo wafanyakazi wa NMB
waliwakabidhi zawadi hizo ikiwa ni moja ya kuadhimisha wiki ya wateja wa
benki ya NMB na kuwapatia somo la kujiwekea akiba kwa kuwataka watoto
wawahimize wazazi kuwafungulia akaunti kwenye benki ya NMB.
No comments: