Mtandao wa Facebook kuzingatia uadilifu kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 28, 2020
MTANDAO wa Facebook umetangaza dhamira yake ya dhati ya kuhakikisha na kuzingatia uadilifu kuelekea uchaguzi mkuu Tanzania,Oktoba 28,2020, ikiwa ni kuhakikishamaadili yanakuwepo kulinda na kuendeleza Demokrasia.
Hata hivyo Mtandao wa Kijamii wa Facebook imezindua njia zitakazosaidia kuzuia kuenea kwa upotoshaji wa habari za siasa au uingiliaji wa masuala ya Uchaguzi Mkuu lakini njia hizo zitaimarisha ushiriki wa wananchi katika masuala ya kisiasa.
Masuala yahusianayo na uadilifu wa mtandao wa Facebook kwenye uchaguzi mkuu ni haya ufanikisha ushiriki wa kisiasa kama njia mojawapo ya kujenga jamii yenye uelewa na ushiriki sahihi katika masuala ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu huu wa Oktoba, Facebook itazindua ujumbe maalum kuwakumbusha watanzania siku ya kupiga kura, ujumbe utakaokuwa ukipatikana katika kurasa za habari za Facebook na Instagram.
Ujumbe huo utakuwa na taarifa rasmi muhimu za upigaji kura na ni shirikishi kwa kwa watumiaji wa Facebook kwa kuwa unawaruhusu kuusambaza ujumbe huo kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii kwa njia ya picha kwenye profile zao.
Pia watanzania wataweza kusambaza picha zinazoonesha furaha yao ya upigaji kura hatua itakayohamasisha ushiriki wa watanzania wengine kwenye uchaguzi mkuu.
Pia Facebook na Instagram kuzindua stika maalumu kuhusu uchaguzi iliyochorwa na na msanii wa kitanzania Othman Mashaushi kwaajili ya Kukabiliana na upotoshaji na habari danganyifu katika Mtandao huo unatambua madhara upotoshwaji wa habari hasa wakati wa Uchaguzi Mkuu na ndio maana Facebook imeshirikiana na shirika la Pesa Check ambalo ni huru katika ufuatiliaji wa taarifa.
Shirika hilo litakuwa na jukumu la kupitia ufanisi wa taarifa zinazotumwa kwenye kurasa mbalimbali za Facebook na Instagram ambapo iwapo ikibainika mahudhui yaliyopostiwa kwenye mtandao kuwa ni ya uongo yatashughulikiwa.
Habari hiyo inazuiliwa kusambaa kwake ili kuizuia habari hiyo isiendelee kupotosha jamii na wakati huo huo habari sahihi zinazoendana na habari husika itakayotajwa kupotosha zitatafutwa na kupostiwa ili kuifafanua.
Facebook imezindua kampeni itakayowawezesha watanzania kuamua wenyewe nini cha kusoma, kuamini na kusambaza kwa wengine.
Kuongeza uwazi kwenye matangazao ya kisiasa, Facebook inaamini kuwa mijadala ya kisiasa inapaswa kuwa wazi kwa kila mpiga kura ndio maana kampuni imeanzisha njia inatoa taarifa zaidi kuhusiana na matangazo ya kisiasa
kwenye Facebook na Instagram, Mapema mwaka huu Facebook ilitangaza ulazima wa uwepo wa uwazi kwenye matangazo hayo ya kisiasa na matokeo yake kila anayetaka kutoa tangazo lihusianalo na siasa wanapaswa kuthibitishwa kuwa wao ni kina nani na kama wanaishi Tanzania.
Zaidi ya hapo Facebook inaongeza ufuatiliaji zaidi kuhakikisha kuwa tangazo husika linaendana na sera huku tangazo hilo likiwekewa alama kuonesha kuwa limelipiwa ili kuwapatia mwanya wananchi kujua ni nani aliyelilipia.
Kila tangazo la kisiasa linalotangazwa Tanzania kwa kipindi hiki linawekwa kwenye maktaba ya matangazo ya ili wananchi wayaone matangazo yaliyokuwa yakioneshwa, watu wa aina gani wameyaona matangazo hayo na kiasi gani cha fedha kilitumika.
Kuwahakikishia wananchi matumizi salama ya mitandao yetu ni kipaumbele kikubwa kwetu hasa wakati wa uchaguzi mkuu.
Vigezo vya Facebook vinavyoendana na matakwa ya kijamii vina masharti Madhubuti yanayolenga kukabiliana na uhalifu, machafuko, kauli chochezi zenye kuamsha chuki kwa wananchi, kuathiri haki ya mpiga kura na usumbufu wa aina yoyote.
Watanzania wanaalikwa kutumia mfumo uliowekwa na Facebook kutoa taarifa kuhusiana na watu wanaosambaza maudhui yanayokiuka masharti yetu hayo ili timu ya Facebook iweze kuyafanyia uchunguzi mahudhui hayo na kuyaondoa.
Kidunia, Facebook imeongeza idadi ya watu wanaoshughulikia usalama wa matumizi ya mtandao wake huo kufikia hadi 35,000 ikijumuishwa na wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili.
Akizungumzia zaidi kuhusiana na jitihada hizo za Facebook, Mkuu wa Sera za Jamii wa Facebook kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika, Mercy Ndegwa, alisema, "Tunafurahia kazi zetu Tanzania. Kama kampuni tumewekeza pakubwa kuhakikisha kwamba Facebook ni sehemu watu wanajiskia salama, wanapata taarifa sahihi na sauti zao zinaskika. Tunaamini kwamba kazi tunayoifanya kuhakikisha uadilifu wa uchaguzi Tanzania itasaidia kupunguza usambazaji wa habari potofu, kuzuia uingiliaji wa uchaguzi na kukuza ushiriki wa raia."
No comments: