MPIGA KURA NI NANI?



Na Avila Kakingo, globu ya jamii
TUME ya Uchaguzi nchini (NEC) imesema kuwa Raia yeyote wa Tanzania aliyejiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura na ana kadi ya kipigia kura iliyotolewa na tume hiyo ana haki ya kupiga kura na kumchagua kiongozi anayemtaka.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Saalam wakati wa Mkutano wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa w Dar es Salaam (DCPC), Afisa Elimu kwa Mpigakura wa NEC, Nuru Liwa amesema kuwa anayetakiwa kupiga kura awe mkazi wa kawaida wa eneo analotaka kupiga kura au amehamia na taarifa zake zimehamishiwa katika kituo anachotaka kupiga kura.

Licha ya hayo Nuru amesema kuwa muda wa kupiga kura Oktoba 28, 2020 ni kuanzia saa moja  kamili (1:00) asubuhi hadi saa kumi (10:00) kamili jioni kwa Tanzania bara na kwa Tanzania Zanzibar vituo vitafunguliwa saa moja kamilia (1:00) asubuhi na kufungwa saa kumi na moja kamili  (11:00) Jioni.

Nuru pia ametaja mambo ya kuzingatiwa kuwa ni mpiga kura anatakiwa kufika kituoni muda uliotangazwa na Tume ya Uchaguzi na muda wa kupiga kura ukiisha hakuna mtu yeyote ataruhusiwa kupiga kura.

Na kama muda wa kupiga kura umeisha na watu bado wapo kwenye mstari Askari wa Kituo atasimama  nyuma ya mtu wa mwisho mpaka wote wamalize kupiga kura.

Hata hivyo ametoa tahadhari kwa wanachama wa vyama vyote kuwa mtu yeyote hatakiwi kuvaa nguo zinazoashiria itikadi ya chama chochote cha siasa.

Licha ya hilo Tume ya Uchaguzi imezingatia watu wenye ulemavu, Mama wajawazito na watu wenye watoto wachanga walioendanao kituoni hapo, wazee na wagonjwa wapewe kipaumbele.

Ikiwa hulioni jinalako katika orodha ya wapiga kura Nuru amesema kuwa mpiga kura anatakiwa amwone karani mwongozaji wapiga kura ili amsaidie kupata maelekezo au kumwonesha kituo  cha mpiga kura.

Licha ya hayo  Nuru amesema kuwa kituo ulichojiandikishia na kupata kadi ya mpiga kura na mahali ambapo jina lako litaonekana. Tume itabandika orodha ya wapiga kura kituoni siku nane (8) kabla ya uchaguzi  yaani kesho.

Kura yako, Sauti yako, nenda kapige kura

No comments: