CCM YAJIVUNIA MTAJI WA WANACHAMA MILIONI 22 WALIONAO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 28
*Ajivunia kampeni za kisayansi wanazozifanya
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
WAKATI zikiwa zimebaki siku 10 kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu Oktoba 28 mwaka huu, Chama Cha Mapinduzi(CCM) kinajivunia idadi ya watu milioni 22 ambao ni wanachama watakaopiga kura huku kina mtaji wa asilimia 75 ya ushindi na hiyo na kabla ya kufanyika kwa kampeni za uchaguzi huo.
Akizungumza leo Oktoba 17, 2020, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Humphrey Polepole amesema kampeni zinaendelea vizuri na kwa kweli kama kuna kitu wanamshukuru
Mungu na na umma wa Watanzania ni kampeni ya mwaka huu wa 2020 ambayo iko tofauti kidogo na wako vizuri Amefafanua Dk.John Magufuli alipoingia madarakani alikuwa na kazi mbili , kazi ya kwanza ni kufanya mageuzi makubwa kabisa ya CCM ili kuhakikisha inakuwa daraja kati ya wananchi na Serikali waliyoichagua.Jambo la pili ni kuhakikisha CCM
inakuwa taasisi ya kulinda maslahi ya wananchi wa Tanzania , Chama ambacho ni imara na kinaweza kuisimamia Serikali kutekeleza yote ambayo umma umewatuma kufanya.
"Kwa hiyo Dk.Magufuli amefanya mageuzi makubwa kutoka Mmutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM ulioketi mwaka 2016 ukifuatiwa na mikutano kadhaa ya Halmashauri Kuu ya mwaka 2017 na hatimaye mkutano mkuu wa CC
M Taifa uliofanyika Desemba mwaka 2017.
"Ambao pia ulisababisha mabadiliko kadhaa kama kufanya mabadiliko ya Katiba ya Chama kama sehemu ya kufanya mageuzi makubwa kwa misingi ya chama chetu, kama uaminifu, uadilifu, unyenyekevu kwa watu na kuchukia na kukemea rusha na aina yoyote ya ubadhirifu pamoja na kupigania maslahi ya wananchi hasa wanyonge
"Hivyo mageuzi hayo yalilenga kuangalia hapa na mtakumbuka tulifanya mabadiliko ya Katiba kwa kutambua ngazi ya msingi ni CCM kwa kuangalia nyumba 10 za mabalozi wa CCM lakini kwa ukweli tulikuwa tunahesabu nyumba , na mnafahamu makazi yetu yalivyo.
"Kwa hiyo mageuzi hayo yalihusisha kutambua ngazi ya msingi ya shina ambalo lina mwana chama mmoja mmoja na tulichobaini wana CCM walihamasika sana kuona chama chao kinauhuisha uhai wa Chama.Hivyo hapa ninaposema wanachama imeongezeka.Mwaka 2015 walikuwa milioni nane lakini leo hii Oktoba 17 mwaka 2020 wamefikia wanachama milioni 17,"amesema Polepole.
Amefafanua wana CCM hao wanafahamiana kuanzia kwa ngazi ya shina, kata , jimbo, wilaya, mkoa na taifa ambapo Dk.John Magufuli yupo."Kwetu sisi ni heshima kubwa ambayo wananchi wametupatia lakini ni heshima zaidi kuongeza idadi ya wanachama mara dufu ya iliyokuwa awali,"amesema.
Polepole amesema hatasema mikakati kwa kina ya ushindi lakini jambo mojawapo ambapo wamelifanya kwa ngazi ya shina kuna watu watano wanatoa uongozi wa wanachama na ngazi ya tawi ndio kubwa kabisa kwani wana kila kitu na ngazi ya kata ndio kubwa zaidi.
"Mageuzi hayo makubwa yameiwezesha CCM kuwa na rasilimali, kuwa imara na kubwa zaidi kuwa na viongozi waaminifu na waadilifu ambao wanautumikia uma watanzania.Ninachotaka kusema katika kampeni hizo zipo ambazo zinapigwa na viongozi na zipo zinazofanywa na wanachama.
"Kampeni ya viongozi inaanzia ngazi ya shina ambayo yenyewe ina viongozi wanne na ndio kamati ya uongozi wa shina ambao hao wanakuwa na wenzao , wanamfikia kila mwananchi katika kila eneo la Tanzania.Ikumbwe CCM ina uongozi wa kata nyingi zaidi kuliko kata za kiserikali, kwa hiyo tukisambaa tunasambaa katika kata zote na ziada na ile ziada inarudi kuongeza nguvu kwingine,"amesema.
Ameongeza halafu kuna kampeni inayofanywa na wanachama , mashabiki n
a wafuasi ambao hao huwaambii kitu zaidi ya CCM hata kama hawana kadi, hivyo wanachama wamekubaliana katika kila wanachama watatu wapeleke mtu mmoja na hiyo ni nje ya mikutano inayoendelea."Kila wana CCM watatu waletee mtu mmoja,
"Watu milioni 15 wakileta watu watatu tutakuwa tumepata watu milioni tano na hivyo ukichukua milioni tano na ukajumlisha na wanachama tulionao milioni 17 unapata watu milioni 22 na hiyo ni kabla ya kupiga kura , hapo hatujafanya kampeni , tayari tuna watu milioni 22 kura zao zimetulia.
"Kwa CCM kabla ya kupiga kampeni tutakuwa na asilimia 75 ya ushindi na hiyo ni kabla ya kupiga kampeni na Kamati ya kampeni ilikuwa imejiwekea malengo yake kura za urais asilimia 90, kwa hiyo sasa hivi kampeni ambazo zimepigwa kwa umaridadi mkubwa na zimepigwa kisayansi kwa viongozi kwenda pande mbalimbali, tutashinda sana katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
"Na utafiti wa kisasi uliofanyika Februari mwaka huu uliotoa matekeo yalionesha mgombea wetu Dk.Magufuli angeshinda kwa asilimia 90, wabunge wangeshinda kwa asilimia 75, madiwani asilimia 80.Kwa Rais wa Zanzibar angeshinda kwa zaidi ya asilimia 75, wawakilishi inagonga zaidi ya asilimia 75 na madiwani asilimia 80,"amesema Polepole.
Amefafanua kuwa utafiti huo ulifanyika kabla ya Corona haijaingia na baada ya Rais Magufuli baada ya kumtanguliza Mungu katikati ya Corona licha ya bezabeza ya wapinzani leo Tanzania ndio nchi pekee ambayo haina Corona."Ndio maana watalii kote nchini wanaendelea kuja Tanzania , uchaguzi wa mwaka huu ushindi wa CCM ni mkubwa sana.
"Chukua ushindi wa ndugu Magufuli wa asilimia 90 wa Februar halafu jumlisha na kishindo cha Corona kutokana na Rais kuwa mstari wa mbele kwa kuwataka watanzania kumlilia Mungu halafu akasema tumshukuru Mungu kwa siku nyingine tatu na sisi ni mashuhuda Tanzania hakuna Corona.Hivyo ukichukua asilimia 90 kisha ukaongeza na ushindi wa Corona na kumshukuru Rais kwa kazi anayofanya , tutashinda sana,"amesema.
Ameongeza na hapo tayari wana mtaji wao wa asilimia 75 ya ushindi na hiyo ni kabla ya kuingia kwenye kampeni.CCM itabaki kuwa na amba moja huku akielezea jinsi ambavyo mikutano yao imefanyika asubuhi kwa zaidi ya asilimia 90 na ilikuwa inajaza watu wengi.
No comments: