BARCELONA YAENDELEA KUJIIMARISHA
Na Piason Kayanda-Michuzi Tv
Fc Barcelona imewaongeza mkataba wachezaji wake Marc-Andre Ter Stegen, Gerard Pique, Clement Lenglet na Frenkie De Jong.
Gerard Pique amesaini kandarasi ya miaka minne na Marc-Andre Ter Stegen amesaini mkataba wa miaka mitano, Clement Lenglet na Frenkie de Jong nao wamesaini mkataba wa miaka mitano utakao waweka katika klabu hiyo mpaka mwaka 2026.
Barcelona imetangaza kuongeza muda wa mkataba kwa wachezaji wanne wa kikosi cha kwanza, pamoja na beki wa kati mwenye uzoefu Gerard Pique ambaye atakakipiga mpaka 2024 hii itamfanya Pique kutumikia klabu ya Barcelona kwa miaka 16.
Mchezaji huyo wa Uhispania Umri wa miaka 33, aliyewasili katika klabu ya Barcelona kutoka Manchester United mnamo 2008, alitolewa nje kwa kadi nyekundu katika ushindi wa 5-1 wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Ferencvaros ya Hungary Jana usiku.
No comments: