WAZAZI WAJITOKEZA KWENYE KLINIKI MAALUM YA WATOTO WENYE VICHWA VIKUBWA NA MGONGO WAZI

 Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akizungumza na wazazi wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi waliofika katika Taasisi ya MOI kwenye mafunzo pamoja na kiliniki maalum iliyoandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya kuanzishwa kwa MOI.

Mfanyabiashara Azim Dewj akizungumza na wazazi wa watoto wenye vichwa vikubwa waliojitokeza MOI leo katika kliniki maalum.

Moja ya mzazi aliyeshiriki kwenye kliniki maalum ya watoto wenye vichwa vikubwa iliyoandaliwa na MOI akichangia jambo.
 TAASISI ya mifupa Muhimbili  (MOI) imeandaa kliniki maalum kwa Watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi ambapo zaidi ya Watoto 120 wamehudhuria na kupewa elimu juu ya matibabu na huduma nyingine kwa Watoto hao.

Mkurugenzi Mtendaji wa  MOI Dkt. Respicious Boniface amesema imeendelea kuboresha huduma kwa Watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi kwa kuwapa kipaumbele cha hali ya juu wanapokuja kupata huduma.

“Tumeanzisha wodi maalum, chumba maalum cha upasuaji ambacho kwa mwezi kinawafanyia upasuaji Watoto kati ya  80 hadi 100 na kwa mwaka ni zaidi ya watoto 1200”alisema Dkt. Boniface.

Dkt. Boniface amesema serikali itaendelea kuwapa huduma bora watoto hao ili wakuwe kama Watoto wengine na kulitumikia taifa. ,Pia alitoa pongezi za dhati kwa wazazi kutokana na ushirikiano wanaonesha kwa madaktari. 

Mfanyabiashara Azim Dewji ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo amesema Tanzania ni nchi ya kipeke ambayo Mungu ameibariki, kwani madaktari wanaupendo kwa wagonjwa na wanashirikiana nao.

“Inatia moyo kwamba madaktari hapa ni wazuri wanafanya kazi kwa upendo hivyo msiwe na wasiwasi mtapona, pia tumshukuru Mungu ugonjwa wa corona haupo nchini kwetu” alisema Azim  Dewji.

Wazazi wenye watoro wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi waliofika MOI wameushukuru uongozi wa MOI kwa huduma nzuri na moyo wa upendo kwa wagonjwa wanaofika kupata huduma kwani wamekuwa wakipata faraja kubwa kutoka kwa madaktari.

No comments: