WAKULIMA WATAKIWA KUACHA KUFANYA KILIMO CHA MAZOEA



Na Woinde Shizza , Michuzi Tv ARUSHA 
Wakulima hapa nchini wametakiwa kuacha kulima kilimo Cha mazoea Ili kuweza kuepuka hasara wanazozipata Mara kwa Mara badala yake walime kwa kuzingatiwa mwenendo wa soko.

Hayo yamebainishwa na mtafiti kilimo biashara kutoka Shirika linalohusiana na utafiti mimea ya asili ya mbogamboga na matunda (world Vegetable Center) lililopo Wilayani Arumeru mkoani Arusha Judith Asenga ambapo alisema wakulima wengi wamekuwa wanalima kwa mazoea ,wame kuwa wanalima bila kuzingatia walime Nini kwa wakati gani wengi wanalima kwa mazoea ya kuangalia mwezi huu wanalima Nini na kwa wakati gani.

Alisema ili mkulima aweze Kulima na kupata faida ni vyema kuanza kuangalia soko na kulitambuwa Kisha akahanze Kuzalisha, kwenda Sokoni na kupata taarifa ya zao gani linaweza kuwa na Uhaba miezi tofauti tofauti ijayo

"Mara nyingi hunakuta mwezi wa nne na watano wakulima wengi wanalima nyanya na Vitunguu lakini kuna mazao mengi ambayo wangeweza Kuzalisha kwa kipindi hicho wangeweza kupata faida, kwaiyo Wakulima Kama wanataka Kulima na kupata faida wanatakiwa waanze kwanza kuingia Sokoni na kupata taarifa za mwenendo wa Soko uzuri wafabiashara wengi wanafahamu ni zao gani halitakuwepo kwa wingi Sokoni kwa kipindi Cha miezi tofauti tofauti kwa mfano Kama Vitunguu na nyanya hunakuta kwa kipindi Cha mwezi wa 12 wa kwanza na wa pili sio vingi Sana Sokoni Kama mwezi wa Saba na nane kwa sababu mwezi wa saba na nane unakuta wakulima wengi wanalima mwezi wa nne na watano ambapo wanapo vuna na kuongiza Sokoni hunakuta wameshatengeneza mafuriko ya mazao ambayo yanasababisha bidhaa zao kuhuzwa kwa Bei ya chini." Alibainisha Judith

Alibainisha kuwa wakulima wazingatie kuangalia soko kabla ya wao kuzalisha na soko ndio lihamue nini mkulima anatakiwa azalishe ambapo alifafanua sio vyema mkulima aanze kununua mbegu Kabla ya kufanya utafiti wa kuongea na Wafanya biashara ,wanunuzi wa mbalimbali wa Mazao mbalimbali ambapo utajua Nini uzalishe na kwa wakati gani.

Aliwataka wakulima kujiunga na vikundi ili waweze kupata fursa mbalimbali ikiwepo elimu mbalimbali ,mikopo huku akibainisha wanapokuwa kwenye vikundi kunawezesha kufikiwa kwa urahisi na kupewa fursa mbalimbali za kuhimarisha kilimo Chao ambacho kina imarisha vipato vyao .

Akiongea na waandishi wa habari moja wa wakulima kutoka katika kikundi Cha vijana nganana manyata wakulima wanaosimamiwa na shirika hilo Eliud Akyo aliitaka Serikali kupeleka maafisa kilimo vijijini Ili wakawape elimu zaidi ya kilimo wakulima wa vijijini nao waweze Kulima na kufanikiwa.

Alisema shirika hili limeweza kuwasaidia wameweza kujua Kulima kwa kufuata msimu kitu ambacho awali walikuwa hawakijui kwani Kabla ya kupata elimu hii walikuwa wakulima kilimo Cha mazoea ambacho kulikuwa kinawasababishia hasara za Mara kwa Mara .

"Kama Mimi shirika hili limeweza kunisaidia nikapata elimu ya kuhifadhi kumbukumbu wakulima wengi wamekuwa wanalima lakini hawahifadhi kumbukumbu kitu kinachomfanya mkulima akilima asijue amepata faida gani na asara gani nanaupenda niwasihi wananchi wenzangu wawekeze kwenye kilimo kwani ukiwekeza kwenye kilimo kunakusaidia kupata faida kubwa na hautakuya mradi ufate mashariti"alisema Agnes's Ndossi

550Mkurugenzi Mtendaji Shirika la linalohusiana na utafiti mimea ya asili ya mbogamboga na matunda mkoani hapa (world Vegetable Center) Dkt.Gabriel Rugalema wa kwanza kushoto akimuonyesha mkurugenzi wa TAHA Jackline Mkini baadhi ya vyakula vilivyotengenezwa na mbogamboga ikiwemo keki jana wakati mkurugenzi huyo wa Taha alipotembelea shirika hilo

016 picha ikionyesha Mtafiti wa maswala ya utunzaji wa mbogamboga kutoka World Vegetables center Alaik Laizer akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari namna ya kuhifadhi nyanya Mara baada ya kuzivuna wakati akizipeleka Sokoni 

258 picha ikionyesha mtafiti kitengo Cha lishe kutoka shirika la World Vegetables center Inviolate Dominick akionyesha baadhi ya matunda yanayolimwa na shirika hilo na kueleza faida zake

412 picha ikionyesha Mtafiti wa kilimo biashara na uchumi kutoka shirika la world Vegetables center Henry Mvungi akiwapa elimu waandishi wa habari jinsi anavyowafundisha wakulima kufanya kilimo biashara.
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la linalohusiana na utafiti  mimea ya asili ya mbogamboga na matunda mkoani hapa (world Vegetable Center)  Dkt.Gabriel Rugalema  wa kwanza kushoto akimuonyesha mkurugenzi wa TAHA Jackline Mkini  baadhi ya vyakula vilivyotengenezwa na mbogamboga ikiwemo keki jana wakati mkurugenzi huyo wa Taha alipotembelea  shirika hilo

No comments: