TAKUKURU KIBITI YAOKOA MAMILIONI YA FEDHA ZA WAKULIMA WA KOROSHO KIBITI


Na Mwandishi Wetu,Kibiti

OFISI ya Mkuu wa Wilaya Kibiti na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) wilaya YA Kibiti imeokoa kiasi cha fedha Sh. 44,054,040 za  wakulima wa korosho wa vyama vya ushirika Mwambao Amcos na Ruaruke Amcos vya Wilaya ya Kibiti za  mauzo ya korosho  msimu wa mwaka 2019/2020.

Mkuu wa wilaya ya Kibiti mkoani Pwani Gullam Hussein Kiffu  akitoa taarifa ya kuokoa fedha za wakulima wa korosho Kibiti alisema korosho za vyama hivyo ziliuzwa katika mnada wa Januari 24,  2020 kwa kampuni ya RV. EXPORT zikiwa jumla ya kilogramu  157,591 ambapo baada ya korosho kuuzwa mnunuzi alichukua jumla ya kilo 71,845 na kuacha kilo 85,746 ambapo korosho zilizobaki ziliendelea kukaa ghalani hadi Takukuru na ofisi ya mkuu wa wilaya ilipofuatilia suala la wakulima wasiolipwa hali zao wapate.

Aidha baada ya ufuatiliaji kuanza ilibainika kuwa mnunuzi wa korosho alikuwa ameshalipa fedha CORECU kwa ajili ya wakulima wa Mwambao na Ruaruke na baada ya fedha hizo kulipwa hazikuwafikia wakulima walengwa  badala yake CORECU walizipeleka kwa wakulima wengine wasiohusika.

"Swala hili liliendelea kufuatiliwa na Ofisi ya TAKUKUKURU na tarehe 28/08/2020 kikao cha pamoja ambacho kilishirikisha ofisi ya mkuu wa wilaya TAKUKURU ofisi ya Mkurugenzi na viongozi wa amcos husika tulikaa kwa pamoja na ndipo ilipoamuliwa kwamba CORECU wawalipe wakulima fedha zao ndani ya siku 14,"amesema Kiffu  na kuongeza kuwa

"Napenda kuwajulisha kuwa CORECU wametekeleza kilichoagizwa na wamelipa kiasi cha shilingi 44054040 ambapo mnaziona hapa na nyingine tayari tumeshawalipa wakulima."

Kiffu aliongeza kuwa zoezi la ufuatiliaji fedha za Wakulima wa korosho lilianza tangu mwezi Novemba 2019 ambapo hadi leo shilingi milioni 300920780 zimeokolewa na kulipwa kwa wakulima ambao walikuwa hawana tena matumaini ya kupata fedha zao.

Alitoa mwito kwa  viongozi wa AMCOS na CORECU kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa ili kuepusha hujuma kwa mazao ya wakulima wanyonge ambao wanatumia gharama kubwa kwenye Madawa lakini baada ya mavuno fedha zao au mauzo yao yanahujumiwa na Watu wachache.

"Lakini pia makampuni ya ununuzi wa mazao ya wakulima wa Kibiti nawaasa kuacha ujanja ujanja wa kuwadhulumu wakulima badala yake fuateni sheria kanuni na taratibu kwani mtajikuta mnaingia katika matatizo ambayo yatayumbisha biashara, "alisema Kiffu.

Alisema TAKUKURU inataka kuwaona wananchi wanyonge wa chini wakitendewa haki na pia wakipata haki zao kwa wakati jambo Mh Magufuli amekuwa akilipigia kelele kila siku na kulitekeleza kwa vitendo.

Awali Kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Kibiti Anna Shine alisema walipokea malalamiko  kutoka kwa vyama viongozi wa Ruaruke Amcos na Mwambao Amcos kuwa baadhi ya wakulima wanadai fedha zao na walienda hadi ofisi ya mkuu wa wilaya na wao walianza kushughulikia madai hayo.

"Korosho ziliuzwa  kwa kampuni ya RV ambaye alizibeba nusu nyingine akaziacha kwamadai ya changamoto ya Barabara na ubovu wa korosho lakini cha kushangaza Ofisi YA mkuu wa Willy's alifanya mnada mwingine na mnunuzi huyohuyo akaja tena kuzikagua na kukubali kuzichukua.

" Ambapo wakulima walikubali wakatwe kufidia ubovu wa barabara kwa kutoa shilingi 80 kwa kila kill fedha Ilizoingizwa  kwenye akaunti YA CORECU lakini CORECU wakijua walichokifanya walichukua fedha hizo hizo kuchepushwa na kupeleka kwa wakulima wengine ambao si walengwa, ".alisema Anna.

Hata hivyo alisema walikaa Pamoja na uongozi wa chama kikuu cha msingi Mkoa wa Pwani CORECU na Amcos jitihada zilizosaidia kubaini fedha zilipopelekwa ambazo zimerudishwa na kupewa wakulima. walengwa. 

Amesemaa kwamba  wanachi wa Kibiti waitumie vizuri ofisi yao  kwani wananchi wengi wamepata haki zao kupitia ofisi hiyo.

"Tutaendelea kuchapa kazi kwa kasi hii hii ili tuweze kutokomeze rushwa na hujuma wanazofanyiwa wakulima wetu wa Kibiti. 




No comments: