SERIKALI YATATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MAJI LONGIDO
Wataalamu wa Wizara ya Maji wakikagua mto Simba ambao ni chanson cha maji ya mradi wa Longido
Mwalimu Anna Revocatus wa Shule ya Sekondari Longido akichota maji kwenye bomba la maji ambalo linahudumiwa na mradi wa maji wa Longido.
Tenki la maji linalohudumia mji wa longido
Wataalamu wa Wizara ya Maji wakishuhudia mwenendo wa maji walipotembelea chanzo cha maji cha mto Simba.
Bwana Abel Kundael akita shaman quake. shamba hili linahudumiwa na maji ya mradi wa maji Longido.
………………………………………………………………………
Na Evaristy Masuha
Serikali kupitia mradi wa maji wa Longido imewezesha upatikanaji wa maji katika mjii waLongido na kijiji cha Engikaret kwa asilimia mia moja. Baada ya kukamilisha utekelezaji wa mradi wenye thamani ya shilingi biloni 14.6 ambao unapokea maji kutoka chanzo cha Mto simba, na umekamilika mwezi Machi mwaka huu.
Akizungumza na Wataalamu wa Wizara ya maji waliopo katika ziara ya kukagua na kutathimini maendeleo ya miradi ya maji katika mkoa wa Arusha mhandisi,Salum Rasul kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya majisafi Arusha (AUWSA) alisema mradi huo ni mkombozi kwa wakazi wa Longido na kijiji cha Engikareti maeneo ambayo yalikuwa na changamoto ya huduma ya majisafi na salama.
“Mradi ulitekezwa kwa lengo la kuongeza huduma ya maji kutoka asilimia 15 ambayo ilikuwa inawezesha wakazi 2,510 mwaka 2017 hadi asilimia 100 sawa na wakazi 16,712 waliopo sasa katika mji wa Longido. Pamoja na wakazi 1,294 wa kijiji cha Engikaret.
Alisema mradi huo umezingatia taratibu zote za afya. Ikiwemo kuhakikkisha maji hayo hayana madini ya Floride yanayozidi kiwango. Akibainisha kwamba hiyo ni hatua nzuri kwa maendeleo ya wananchi wa Longido na Mkoa wa Arusha kwa ujumla.
Nae mkuu wa msafara wa wataalamu waliotoka Wizara ya Maji, Ingrid Sanda alisema serikali imejipanga kuhakikisha inamtua mama ndoo ya maji kama ilivyo ahidi. Huku akiwataka wakazi wa maeneo hayo kuhakikisha wanailinda miundombinu ya maji ili isiharibike.
Kwa upande wake Anna Revocatus ambae ni mkazi wa Longido alisema maji hayo yamewawezesha kubadili maisha kwa kuanzisha kilimo cha bustani na kuwezesha mazingira yakupendeza.
” Kwa kweli nina miaka kumi hapa. Nimekuwepo wakati mji unapambana na changamoto ya upatikanaji wa maji. Hali ilikuwa Mbaya sana. Nashukuru kukamilika mradi huu wa maji, sasa hivi naweza kufanya kazi zangu kwa uhakika. Nimeweza kulima bustani ya Mbogamboga, matunda, na ninajipanga kuanza kilimo cha kisasa cha bustani kwa kutumia maji haya,” Anna alishukuru serikali.
Mwananchi mwingine, Abel Kundaeli alisema ameanzisha shamba la vitunguuu na matarajio yake ni kuuza ndani na nie ya nchi. Akiongeza kusema kwamba kwa sasa shamba hilo limetoa ajira kwa watu kumi na anatarajia kupanua zaidi.
Kuhusu gharama za maji Abel alisema ni nafuuu sana ukilinganisha na soko la bidhaa za kilimo katika miji ya Arusha na chi jirani ya Kenya. Kwahiyo hana wasiwasi na mapato.
No comments: