Serikali mbioni kujenga kiwanda cha dawa za Binadamu mjini Makambako

Na Amiri Kilagalila,Njombe
SERIKALI mkoani Njombe imekamilisha zoezi la uthamini ili kuanza mchakato wa ulipaji fidia kwa wakazi wa kijiji cha Idofi ambao wamepisha eneo lenye ukubwa wa ekari 20 kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha dawa za binadamu chenye hadhi ya kimataifa katika halmashauri ya mji wa Makambako.

Mpango huo umewekwa bayana na mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama cha mapinduzi katika mkoa huo ambapo amesema hatua iliyofikiwa sasa ni wananchi kufungua akaunti benki ili kuwekewa fedha hizo.

Rubirya amesema kukamilika kwa ujenzi huo kutaifanya Tanzania kuzalisha dawa zake yenyewe na kuinua uchumi kwa wakazi wa Njombe na Taifa kwa ujumla.

“Tumekwishatenga ardhi kiasi cha ekari 20,uthamini wa fidi umekamilika.Na wiki ijayo magleda yanaanza kusafisha eneo la Idofi tayari kuanza shughuli za ujenzi wa Kiwanda”alisema Marwa Rubirya

Mratibu wa uchaguzi wa chama cha mapinduzi kanda ya nyanda za juu kuzini Salimu Abri maarufu ASAS ameeleza kwanini watanzania wanapaswa kumpa miaka mingine mitano Rais Magufuli,Wabunge na madiwani wa chama hicho.

“Tumemleta tene Magufuli kwasababu alichokifanya kwa miaka mitano,wachambuzi wa kisiasa wanasema angekuwa Rais mwingine ingebidi afanye miaka 15 au Ishirini”alisema Salimu Abri

Nao baadhi ya wagombea ubunge wa majimbo tofauti ya mkoa wa Njombe akiwemo Deo Sanga, Festo Sanga na Joseph Kamonga wanasema wanakwenda kuzitafuta kura kwa ujasiri kwa kuwa serikali imefanya mambo mengi ambayo yanagusa wananchi.

Dilisha Tayari limefunguliwa kilichobaki ni wagombea kuingia mtaani kuzisaka kura .

No comments: