MGOMBEA UBUNGE MKURANGA ABDALLAH ULEGA AZUNGUMZIA UMUHIMU WA MAWASILIANO KATIKA MAENDELEO


Na Mwandishi Wetu

MGOMBEA  ubunge jimbo la Mkuranga mkoani Pwani Abdallah  Ulega amesema mawasiliano ni jambo muhimu sana kwa jamii, Kwa sababu huleta maendeleo na kufanya uchumi ukuwe.

Ulega ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ameyasema hayo katika Kata ya Magawa wilayani Mkuranga mkoani Pwani akiwa katika mkutano wa kampeni ambapo ametembelea ujenzi wa mnara wa simu unaoendelea katika Kata hiyo na kusema ujenzi huo utarahisisha mawasiliano yawatu na biashara.

Aidha Ulega amesema mpaka sasa minara mitano inajengwa katika wilaya ya Mkuranga ambapo ukiacha kata ya Magawa, Bupu na Mbezi, hivyo ameahidi wanachi kuwa changamoto ya mawasiliano mkuranga inaenda kuwa historia.

Pia mgombea ubunge huyo amesema ukiacha ujenzi wa mnara katika Kata ya magawa ameshatoa ushirikiano Sana katika maendeleo ikiwemo barabara,afya na elimu nakuomba wananchi kukipa tena miaka mitano chama cha mapinduzi ili wakafanye maajabu katika maendeleo.

Hata hivyo Ulega ameongeza  endapo wananchi wa Magawa watamchagua basi ataunga mkono ujenzi wa zahanati ya Makumbea kwa kutoa bati 150 ili kuboresha huduma za afya na kwa upande wa umeme atamsisitiza mkandarasi ili mradi unaondelea katika kata hiyo uwezekukamilika kwa wakati.

Akiwa kata ya Msonga amewataka na wananchi wa hapo kuendelea kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi kwa kukipa kura nyingi na kuwaahidi , kuwa kupitia ilani ya chama watatuliwa changamoto zao za afya, elimu pamoja na miundo mbinu.

Aidha Ulega ameeleza kuwa msonga imekuwa kama kisiwa kutokana na changamoto ya barabara,ambazo nyingi hazipitiki lakini amewatoa hofu wananchi kuwa barabara zote zitafunguka na uchumi utakuwa miongoni mwao.

Kwa upande wake Juma Abeid ambaye ni mgombea udiwani Kata ya Magawa amewambia wananchi mpaka ifikapo Oktoba  mnara huo utakuwa umekamilika na vijiji vyote vitano vya kata hiyo vitaondokana na changamoto ya mawasiliano.
Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga, Abdallah Hamisi Ulega (kulia) akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapindunzi na Wananchi leo katika Kata ya Magawa wilayani mkuranga mkoa wa Pwani. (Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

Wananchi wa kata ya Magawa wakimsikiliza Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga, Abdallah Hamisi Ulega(hayupo pichani)
Wanachapa wapya wakipokea Kadi za CCM
Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga, Abdallah Hamisi Ulega akiwa na viongozi wa kata ya Magawa wakiwa katika eneo linalojengwa mnara huu.
Ujezi wa mnara wa simu katika kata ya Magawa ukinendela kama unavyoonekana pichani.

No comments: