WANAHABARI WAPEWA SOMO LA KURIPOTI HABARI ZA AFYA DAR
Tanzania public Health Bulletin (TPHB) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wamekutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kutoa mafunzo maalumu kuhusiana na namna bora ya kuripoti habari za afya ambapo kupitia mradi wa Takwimu na Sera za afya kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, Wizara ya afya, Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na ofisi ya mganga mkuu wa Serikali wamerahisisha namna ya kupata taarifa muhimu za afya kupitia jarida la Afya ya Jamii nchini, ambalo limesheheni taarifa na matokeo ya tafiti mbalimbali za kisayansi.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara Kuu ya Afya Gerald Chami akizungumza na wanahabari wakati wa mafunzo maalumu ya kuwajengea wanahabari uwezo wa namna ya kuripoti habari za afya, ambapo ameeleza kuwa Wizara hiyo imetengeneza daraja baina yao na waandishi wa habari ili wananchi waweze kupata taarifa muhimu za afya kwa wakati, leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Uratibu na Ukuzaji Tafiti kutoka Taasisi ya utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dkt. Mary Mayige akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mafunzo ya maalumu ya kuwajengea uwezo wanahabari katika kuripoti habari za afya, ambapo amesema kuwa Mamlaka hizo zipo tayari wakati wowote katika kutoa taarifa na ufafanuzi, leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mhariri mkuu wa Jarida la Afya ya jamii Tanzania (TPHB) Dkt.Julius Massaga akitoa somo kwa waandishi wa habari kuhusiana na namna ya kuripoti habari za afya na kueleza kuwa kupitia jarida hilo la Afya wananchi, wanahabari na watunga sera watapata fursa ya kupata majibu ya maswali yao kupitia tafiti mbalimbali zilizochapishwa katika jarida hilo, leo jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa habari kutoka Michuzi Blog Leandra Gabriel akipokea cheti cha ithibati na pongezi mara baada ya kufuzu mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku mbili, leo jijini Dar es Salaam.
Viongozi mbalimbali kutoka TPHB, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari walioshiriki mafunzo hayo, leo jijini Dar es Salaam.
No comments: