Vodacom yazindua huduma ya “Jimixie Bundle”, kumuwezesha mteja kutengeneza mseto wa bando lake mwenyewe anavyopendelea kwa gharama zake.


Mkuu wa Kitengo cha Mikakati na Thamani kwa Wateja Vodacom Tanzania PLC, Jackson Walwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu bando jipya la Vodacom Jimixie linalowapa wateja uhuru na urahisi wa kujitengenezea mseto wa bando zao wenyewe kutegemeana na mahitaji yao, muda wa kuisha kwa bando, motisha na gharama. Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania PLC, Linda Riwa. 
Wafanyakazi wa Vodacom, wateja na wanahabari wakifuatilia tangazo la JIMIXIE BUNDLE lililokuwa likichezwa kwenye screen wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo mpya kutoka mtandao wa Vodacom. 

……………………………………………………..
 Huduma hii mpya inalenga kuwawezesha zaidi wateja.
Dar es salaam. 

Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza kidijitali nchini, Vodacom Tanzania PLC leo imezindua huduma nyingine ya kwanza na ya kipekee katika soko ijulikanayo kama Jimixie bando – Hii ni huduma ambayo inawapa wateja uhuru na urahisi wa kujitengenezea mseto wa bando zao wenyewe kutegemeana na mahitaji yao, muda wa kuisha kwa bando, motisha na gharama.

Akiongea na waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam, wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo mpya, Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara Bi Linda Riwa amesema, kwa miaka mingi kampuni ya Vodacom imeonyesha mfano katika uvumbuzi na kujenga jamii ya kidijitali kwa kuzindua huduma za pekee na za kwanza sokoni kwa sababu ya ari ya kampuni hii ya kufanya maisha ya
wateja kuwa rahisi, bora na yenye utoshelevu zaidi kwa kupitia teknolojia na uvumbuzi.

“Kwa kutambua kwamba mahitaji ya kila mteja ni tofauti na wakati huo huo wateja wote wanahitaji kupata thamani zaidi kwa kile wanachokilipia, tumeamua kutengeneza huduma ambayo inawapa uhuru wa kupata kile wanachohitaji na kwa gharama ambayo wako tayari kuilipa. 

Mteja anaweza akatengeneza bando lake mwenyewe lenye Data, SMS na Dakika za  maongezi kwa pamoja kutegemeana na mahitaji yao, kwa gharama wanayoweza kuimudu na kwa muda wa kuisha kwa bando wanaoutaka. Huu ni ushahidi wa namna ambavyo tunawajali wateja
wetu kwa kuwapatia uhuru wa kutengeneza mseto wa bando zao wenyewe jambo ambalo litawapa urahisi na uhakika katika namna ambavyo wateja wanafanya matumizi yao” alisema Riwa.

Vodacom Tanzania PLC inajivunia kuwa kampuni inayomjali mteja huku ikiwa na aina mbalimbali za bando ambazo zinakidhi mahitaji ya wateja kutegemeana na mahitaji yao mahsusi.

Hata hivyo ni mara ya kwanza kampuni hii inaruhusu wateja wake kujitengenezea bando zao wenyewe kwa gharama yoyote wanayoweza kuimudu ili kuweza kupata kile wanachohitaji.

“Kwa mara ya kwanza nchini, wateja watakuwa na uwezo wa kuchagua ni kiasi gani wanataka kutumia, na wanataka kutumia katika huduma gani.

 Tutaendelea kuzindua huduma zenye ubunifu kwa wateja wetu ili kuhakikisha kwamba wanapata huduma za kipekee kwenye mtandao bora na wa kisasa popote pale walipo wakiwa na Vodacom. Tumefanya hivi kwa ajili ya kurahisisha maisha ya wateja wetu tukiwapa uhuru wa kununua kile wanachotaka kutumia huku wakipata manufaa zaidi katika Data, SMS na matumizi ya dakika za muda wa maongezi,” alihitimisha Riwa.

Akiongelea kuhusu utaratibu wa huduma, Mkuu wa idara ya Mikakati na Thamani kwa Wateja Jackson Walwa amesema kwamba huduma hii inapatikana kwa wateja wote na katika mifumo yote ya simu za kawaida na simujanja kwa kupiga kupiga *149*01#J4U>JIMIXIE BUNDLE,
Mteja atakuwa na uwezo wa kutengeneza bando lake mwenyewe kutegemeana na anataka nini na huduma anayoweza kuimudu.

“Huduma ya JIMIXIE BUNDLE imetengenezwa mahususi kuhakikisha kwamba wateja wetu wote wanaweza kununua bando bila kujali wana kiasi gani; unaweza kununua bando kwa kiasi 

C1: VODACOM PUBLIC 

kidogo cha fedha cha TSH 520, TSH 630, TSH 710, TSH 870 au ukiwa na kiasi chochote cha juu unachotaka. Kwa kifupi hatumuachi mtu nyuma,” alisema Walwa.

No comments: