WADAU WATAKIWA KUONA UMUHIMU KUSHIRIKIANA KUSIMAMIA UTUNZAJI MAZINGIRA YA VYANZO VYA MAJI
NaJusline Marco-Arusha
Wadau wa kidakio cha mto Themi jijini Arusha wametakiwa kuona umuhimu wa kushirikiana katika kusimamia utunzaji wa mazingira ya vyanzo vya maji ili kuweza kupata maji safi na salama.
Akizungumza katika uzinduzi wa jukwaa la watumia maji kidakio cha Mto Themi Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Rasilimali za Maji Bi.Rosemary Rwebugisa kwa niaba ya Mkurugenzi Msaidizi kutoka idara hiyo amesema kuwa lengo la uzinduzi huo ni kushirikisha wadau katika ngazi ya kidakio ili waweze kujadili mikakati ya pamoja inayolenga kuboresha usimamizi
Aidha amesema kuwa bodi ya maki ya Bonde la Pangani ni mojawapo ya mabonde tisa yaliyopo nchini chini ya Wizara ya maji yaliyoanzishwa kwa sheria ya usimamizi wa udhibiti wa matumizi ya maji namba 42 ya mwaka 1974 ambapo sheria hiyo ilifutwa na sheria ya usimamizi wa rasilimali za maji namba ya mwaka 2009 ambayo ndiyo inayosimamia utendaji wa kila siku.
Bi.Rosemary amesema kuwa vyanzo vya maji vimekuwa vikichafuliwa na jamii kwa kufahamu ambapo uchafuzi huo unatokana na shughuli za kibinadamu ikiwemo uchungaji wa mifugo,kilimo,utupaji taka pamoja na baadhi ya madereva wa pikipiki kuosha pikipiki zao pembeni mwa mto au ndani hali inayoweza kusababisha madhara kwa watumiaji wa maji hayo.
Naye mwenyekiti wa watumia maji bonde dogo la Themi Ismael Marunda amesema kuwa bonde hilo huaribiwa na baadhi ya wananchi kwa kukaidi Sheria zilizowekwa juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji ikiwemo upandaji miti ambayo sio rafiki na maji ikiwa changamoto hizo hupelekea vyanzo vya maji kupotea na kupoteza sifa ya watu kuyatumia.
"Mamlaka husikia zikiwajibika kuelimisha wananchi juu ya utunzaji wa mazingira kwani wengine wanafanya kwa kufahamu au kutokufahamu hivyo waelimishwe zaidi wafahamu madhara ya uharibifu wa rasilimaji maji ili mwananchi anayekaidi achukuliwe hatua za kisheria Kama mfano kwa wengine,"alisema Mwenyekiti huyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa bodi ya maji bonde la Pangani linalojumuisha Mikoa ya Arusha ,Kilimanjaro,Tanga na Manyara Segule Segule amesema kuwa jukumu la usimamizi wa rasilimali maji unahitaji ushirikiano wa kila mmoja ili kurahisisha ushirikishwaji kama maelekezo ya sera ya mwaka 2002 inavyohimiza kuwepo kwa ushirikishwaji wa jamii.
"Sisi kwenye Mambo ya rasilimaji maji tunazo jumuiya za watumiaji ambazo zinahuasika na usimamizi wake kwani hii haitoshi lazima kila hatua tuwahusishe wadau mbalimbali kwa kukaa pamoja ili kuepuka mchafuko wa rasilimali maji ambayo imekuwa changamoto zinaotukabili,"alisema Mkurugenzi huyo.
Meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa) mkoa wa Arusha,Injinia Joseph Makaidi ameeleza uharibifu wa rasilimaji maji uliopo katika jamii unaotokana na mahitaji ya matumizi ya maji ya kijamii ambayo hutokea pale rasilimali hiyo inapokosekana katika baadhi ya maeneo hali inayopelekea jamii kufanya uharibifu huo.
Sambamba na hayo mwezeshaji kwenye uzinduzi wa jukwaa hilo,Mtaalamu wa maji chini ya ardhi Godwin Kapama amesema kuwa tafiti zinaonyesha kuwa zaidi ya visima 20 vimechimbwa kiholela hali inayosababisha upataji wa maji yasiyosalama kwa matumizi kutokana na wengi wao kuchimba visima hivyo pembezoni mwa vyoo.
Vilevile ameongeza kuwa ni vyema wadau hao wakatoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kuwatumia wataalamu wa maji katika uchimbaji wa visima vyao ili kuweza upata maji safi na kuepuka uchimbaji holela wa visima.
Hata hivyo Kidakio kidogo cha Mto Themi ni mojawapo kati ya vidakio nane vilivyomo ndani ya kidakio cha Kikuletwa katika bondebla Pangani ambapo eneo kubwa la Mto Themi linapatikana katika jiji la Arusha ambapo vyanzo vyake vya maji vinaanzia kwenye mlima Meru katila kijiji cha Olgilai na kutiririsha maji jiji la Arusha katika umbali wa Kilomita 40 hadi 60.
Sambamba na hayo Mto Themi unajumuisha matawi ya mito iliyopo upande wa juu wa mto ikiwemo Ngaramtoni,Ngarenaro,Sanawari,Sekei,Burka na Kijenge ambapo matawi hayo ya mito yanapita katika jiji la Arusha na maji yake yanatumika katika matumizi madogo na makubwa hali inayopelekea kukubwa na uchafuzi.
Hata hivyo mchakato wa uundwaji wa jukwaa la wadau wa Mto Themi katika utekelezaji wa programu ya maendeleo ya sekta ya maji awamu ya pili, ambapo jukwaa hilo limekutanisha wadau mbalimbali kwa lengo la kujadili,kubadilishana uzoefu,kujifunza,kutoa ushauri,maoni,mawazo na mtazamo juu ya usimamizi na uendeshaji wa rasilimali za maji katika Kidakio husika ambapo pia jukwaa hilo litawasaidia wadau kujadili changamoto mbalimbali zinazohusiana na rasilimalivza maji na kuweka mpango wa pamoja wa utatuzi.

Washiriki wa jukwaa la wadau juu ya changamoto za usimamizi wa rasilimali za maji kwenye Kidakio cha Mto Themi,kutoka katika sekta mbalimbali jijini Arusha.
Rosemary Rwebugisa Kaimu Mkurugenzi msaidizi idara ya rasilimali za maji akizindua jukwaa la wadau wa kidakio cha Mto Themi jijini Arusha.
No comments: