Teknolojia ya kidijitali inavyoweza kuboresha elimu Tanzania



Wiki hii serikali imetangaza mpango wa kutekeleza mkakati mpya unaolenga kuboresha elimu ya sekondari nchini Tanzania.

Akizungumza katika mkutano wa wadau wa elimu jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo alieleza dhamira ya serikali wa kuboresha mfumo wa elimu nchini Tanzania.

Amebainisha kuwa dhamira hiyo inalenga kufanya maboresho kwa kwa kuanza kuzipatia shule vifaa muhimu vitakavyowezesha kuboresha mazingira ya kujisomea na kuhakikisha kuwa wanafunzi wa Tanzania wanajifunza masuala ya teknolojia, elimu ambayo itawasaidia kufanya vizuri katika ulimwengu huu unaokua kwa kasi kiteknolojia.

Mpango wowote wa serikali wenye lengo la kuboresha elimu ni jambo jema lenye kufurahiwa na wengi. Umuhimu wa kuhakikisha kuwa kizazi kijacho kinanufaika na teknolojia na kinakuwa na elimu inayohitajika ili kiweze kufanya vizuri katika ulimwengu wa kiteknolojia halipaswi kuchukuliwa kwa urahisi.

Serikali na sekta binafsi zimekuwa zikishirikiana na kwa muda sasa na zote zina uelewa mkubwa kuhusu jambo hilo.

Suala la kuboresha upatikanaji wa teknolojia ni moja ya ajenda kubwa zaidi za sekta ya mawasiliano ya simu nchini Tanzania, kwa njia ambazo zitawanufaisha zaidi vijana. Kampuni za mawasiliano ya simu Tanzania zimejidhatiti zaidi. Mfano mmojawapo ni Tigo Tanzania ambayo imefanya makubwa sana katika sekta hii.

Mwaka 2016, Tigo iliingia kwenye ushirikiano na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuwezesha upatikanaji  wa huduma za intaneti katika shule za sekondari nchini kuwezesha mfumo wa shule mtandao(eSchool).Hadi sasa, Tigo imeweza kutoa huduma ya intaneti bure kwa wanafunzi zaidi ya 64,000 nchini kote.

Aidha, Tigo imejikita katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaelimika katika sekta ya teknolojia. Kampuni hiyo imekuwa ikifanya shughuli zake kwa kushirikiana na mpango wa Apps na Girls unaowasaidia watoto wankike na wanawake kupata ujuzi wa kiteknolojia ili kuondoa utofauti wa elimu ya kiteknolojia kati ya wanawake na wanaume nchini.

Ushirika huo umewezesha Apps and Girls kuzifikia shule nyingi zaidi na jamii mbalimbali ambapo zaidi ya wasichana 3,000 wamenufaika na mpango huo. Mkakati huo umewezesha kuanzishwa kwa ujasiriamali wa kidijitali na wabunifu wa teknolojia.

Kazi hizi za kampuni kama Tigo na sekta ya mawasiliano ya simu kwa ujumla si haba wala za kubeza kwani kwani zinasaidia kukuza elimu kupitia teknolojia, kuibua ndoto za vijana na kuzifanya kuwa kweli kupitia fursa mbalimbali katika sekta hiyo.


No comments: