MKAZI WA ARUSHA KIZIMBANI KWA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA
Na Karama Kenyunko Michuzi TV.
MKAZI wa Arusha eneo la Wakingori Kisimiri Chini, Kaaneli Akyoo (50) amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha akikabiliwa na shtaka moja la kusafirisha dawa za kulevya
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na upande wa Jamuhuri mbele ya Hakimu Mushi imedai kuwa mshtakiwa ametenda kosa hilo Agosti 19, mwaka 2020 huko katika kijiji cha Kisimiri chini wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
Inadaiwa kuwa siku ya tukio mshtakiwa Akyoo alikutwa akisafirisha dawa za kulevya aina ya bangi zenye uzito wa kilograms 160 huku akijua kuwa kufanya hivyo ni kosa na kinyume cha sheria.
Hata hivyo, mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande hadi Septemba 7, 2020 kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kutajwa. Kwa mujibu3wa upande wa Jamuhuri upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika
No comments: