SHIRIKA LA WORLD VISION WAKABIDHI MRADI WA MAJI HANDENI WENYE THAMANI YA MILIONI 199.1

MKUU wa wilaya ya Handeni Toba Nguvila akikata utepe kuashiria uzindua mradi wa maji mradi wa maji uliojengwa na shirika la World vision hongkong na kusimamiwa na word vision Tanzania katika Kijiji cha Pozo Kata ya Kwamsisi Tarafa ya Kwamsisi wilayani Handeni Mkoani Tanga wenye thamani ya sh.milioni 199,001,976 ambao utawanufaika wananchi 1,709
MKUU wa wilaya ya Handeni Toba Nguvila akionya maji hayo mara baada ya kufanya uzinduzi wa mradi wa maji uliojengwa na shirika la World vision hongkong na kusimamiwa na word vision Tanzania katika Kijiji cha Pozo Kata ya Kwamsisi Tarafa ya Kwamsisi wilayani Handeni Mkoani Tanga wenye thamani ya sh.milioni 199,001,976 ambao utawanufaika wananchi 1,709
Mkuu wa wilaya ya Handeni Toba Nguvila kulia amtwisha ndoo ya maji kichwani mkazi wa Kijiji cha Pozo Mwanahamisi Selemani mara baada ya kuzindua mradi wa maji radi wa maji uliojengwa na shirika la World vision hongkong na kusimamiwa na word vision Tanzania katika Kijiji cha Pozo Kata ya Kwamsisi Tarafa ya Kwamsisi wilayani Handeni Mkoani Tanga wenye thamani ya sh.milioni 199,001,976 ambao utawanufaika wananchi 1,709
MKUU wa wilaya ya Hanadeni Toba Nguvila kushoto akimpongeza Mratibu wa Mradi wa Maendeleo Kwamsisi wa Shirika la World Vision Tanzania Jackline Kaihura wakati wa makabidhiano ya mradi wa maji
MKUU wa wilaya ya Handeni Toba Nguvila akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wa kwanza kulia ni Mratibu wa Mradi wa Maendeleo Kwamsisi wa Shirika la World Vision Tanzania Jackline Kaihura
Mratibu wa Mradi wa Maendeleo Kwamsisi wa Shirika la World Vision Tanzania Jackline Kaihura akisoma taarifa yake kabla ya uzinduzi wa mradi huo

SHIRIKA la World Vision Tanzania limekabidhi mradi wa maji uliojengwa katika Kijiji cha Pozo Kata ya Kwamsisi Tarafa ya Kwamsisi wilayani Handeni Mkoani Tanga wenye thamani ya sh.milioni 199,001,976 ambao utawanufaisha wakazi wa kaya 582 ambayo ni sawa na wanufaika 1,709.

Makabidhiano hayo yalifanywa na Mratibu wa Mradi wa Maendeleo Kwamsisi wa Shirika la World Vision Tanzania Jackline Kaihura kwa Mkuu wa wilaya ya Handeni Toba Nguvila katika Kijiji cha Pozo.

Alisema kwamba mradi huo wa maji katika Jijiji cha Pozo umetekelezwa kwa ufadhili World Vision Hongkong chini ya usimamizi wa shirika la World Vision Tanzania Kwamsisi AP katika mwaka wa fedha 2018/2019 kwa ushirikiano na wataalamu wa maji katika Halmashauri ya Handeni (Ruwasa)

Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo Jackline alisema kwamba mradi huo umetekelezwa na wakandarasi watano ambapo Victoria Drilling Company walichimba kisima kwa kiasi cha milioni 28, 137, 100, Kisomboko Builders Limited walifanya ununuzi na usambazaji wa mabomba kwa kiasi cha milioni 30,500,000.

Alimtaja mkandarasi mwengine kuwa ni Siha Enterprises Limted ambao walifanya kazi ya ujenzi wa tenki na vituo vya kusambaza maji (DPs) wenye thamani ya milioni 62, 260, 670, Kiroi Construction Limted ambao walitengeneza kibanda cha pump chenye thamani ya milioni 15,891,296.

“Lakini wakandarasi wengine ni Best one Limited ambao walifanya ununuzi na uwekaji wa solar Panels kwa kutumia kiasi cha milioni 58,642,460 huku ununuzi wa pump ambao ulifanywa na worldvision ukigharimu kiasi cha milioni 3,570,450”Alisema

Aidha alimueleza Mkuu huyo wa wilaya kwamba ipo miradi mingine ya maji iliyotekelezwa kwa ufadhili wa shirika la worldvision chini ya Kwamsisi Area Program ambayo imekamilika mwaka huu na yote imekamilika kwa mafanikio.

Alisema ni mradi wa maji wa Kijiji cha Kwanyanje ambao uligharimu jumla ya fedha za kitanzania sh.milioni 141, 84,785.76 na mradi wa kukarabati miundombinu ya maji kijiji cha Kwasunga uliogharimu kiasi cha milioni 150,834,540.

“Pia kuna mradi wa maji unaohudumia vijiji vya Kwamsisi na Kwedikabu ambao ulikamilika mwaka 2018 na tayari umewanufaisha wananchi wa vijiji hivyo na wanauendesha wenyewe kwa kupitia vyombo vya watumia maji ambao uligharimu kiasi cha milioni 207.

Awali akizungumza mara baada ya kuzindua mradi huo Mkuu wa wilaya ya Handeni Toba Nguvila alisema ameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo kuanzia hatua ya tenki, koki na maeneo ya kuchotea maji yapo vizuri huku akilishukuru shirika hilo kwa kusaidia juhudi za serikali katika kusaidia kuipatia ufumbuzi tatizo hilo.

Alisema wananchi hao walikuwa wanakunywa maji ya kwenye mabwawa na madimbwi ambayo sio salama kwa afya zao na watoto lakini hivi sasa wakwenda kunywa maji salama yaliyochimbwa kwenye kisima chini ya ufadhi wa Shirika la Wordvision Hongkong wakiwa ni wadau muhimu wa maendeleo kwenye wilaya ya Handeni na hapo Pozo.

“Mradi huu mmeupata ni mzuri na maji ni safi na salama hivyo niwapongeze world vision na wataalamu wa Ruwasa. Lakini wananchi mhakikishe mnaulinda na kuutunza kama mboni ya jicho”Alisema

Hata hivyo alisema ni muhimu mradi huo utunzwe ili uweze kuwanufaisha leo na siku zijazo huku akieleza wakiona watu wanafanya uharibifu viongozi wachukue hatua kali kwa faida ya wananchi wa eneo hilo.

No comments: