Ni Leipzig dhidi ya PSG. Je, nani kuonesha mabavu yake na kufuzu hatua ya Fainali?
BILA shaka fainali ya michuano mikubwa barani Ulaya imekuwa ya aina yake na yenye kusisimua!
Ligi ya Mabingwa kwa namna ya kipekee imetuletea matokeo a mbayo hatukuyatarajia. Burudani, kuibuka kwa miamba mipya, matokeo ya kushtua – haya ni baadhi ya mambo yaliyojitokeza na tumeyashuhudia kwa siku kadhaa zilizopita.
Uhalisia kwamba Juventus na Real Madrid waliishia katika nafasi ya robo fainali, ilitushangaza wengi. Huenda ukawa ni mwanzo tu wa mengi tutakayo yashuhudia msimu huu.
Wataalamu Leipzig na wapambanaji Lyon wamefanikiwa kuweka historia kwenye hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa. Upande wa pili, wakongwe Bayern Munich waliwachakaza Barcelona kwa magoli 8. Haipingiki, itawachukuwa muda Barcelona kupona maumivu haya.
Matokeo ya kushangaza kwenye hatua ya robo fainali yamepelekea kuwa na mpambano wa kimataifa kati ya Ufaransa na Ujerumani kwenye hatua ya nusu fainali: Leipzig kuvaana na PSG, Lyon dhidi ya Bayern Munich.
Usiku wa leo majira ya saa 4 tunafursa ya kuangalia mtanange wa nusu fainali.
Leipzig wameonesha umwamba wao kwa kuwaburuza Atletico Madrid kwenye hatua ya robo fainali katika mchezo uliokuwa na miujiza ya aina yake.
Siku moja kabla ya mchezo huo, ulionekana mtanange wa kusisimua kati ya PSG na Atalanta. Mwisho wa siku vijana kutoka Italia wakaambulia kipigo baada ya Wafaransa kupindua meza zikiwa zimesalia dakika 3 mpira kumaliza na kipenga cha mwisho kikalia wakati PSG akishinda kwa magoli 2- 1!!
Mpaka sasa, Leipzig na Paris Saint- Germain hawajakutana katika mchezo wowote, hii inapelekea kuwa na mchezo wa kuvutia Zaidi. Timu hizi ziliwahi kukutana mwaka 2014 katika mchezo wa kirafiki na Leipzig kuibuka na ushindi wa magoli 4-2.
Timu zote zimeweka historia ya kufika hatua ya nusu fainali!
Tunaweza kusema hii ni mara ya pili kwa Leipzig kushiriki kwenye Ligi ya Mabingwa na wamefanikiwa kujiweka kwenye nafasi ya timu 4 bora Ulaya kwa mara ya pili. Kwa maana hiyo, Leipzig wanakila sababu ya kusherehekea mafanikio haya kama watafika fainali au hata wakiikosa fainali.
Kwa upande wa mwingine, PSG wanaendelea kulisogelea kombe la Ligi ya Mabigwa ambapo hawajawahi kushinda. Baada ya kubadilisha matokeo kwenye mchezo dhidi ya Atalanta, timu ya Tuchel wameonesha umwamba wao na fikra za kibingwa. PSG wanasababu ya kujiamini kwenye mchezo dhidi ya Leipzig.
Aliyepewa nafasi anajulikana na kila mtu, odds zinathibitisha hilo. Ushindi wa PSG umedhaminiwa kwa odd ya 1.77, wakati ushindi kwa Leipzig ni 4.60 na sare ni 3.72.
Wataalamu wa Meridian wamekuwekea ofa ya machaguo zaidi ya 1,200 ambayo unawezakuyaangalia hapa.
Kuwa sehemu ya mchezo huu na ubashiri vile unavyopenda! Kwa odds nzuri, ofa kabambe za michezo na mambo kemkem, Meridian inakusaidia kuwa mshindi!
Jisajili na meridianbet hapa www.meridianbet.co.tz na furaha yako itaanzia hapo. Pakua App ya Meridianbet kwenye simu yako na uanze kubashiri kwa uhuru nyumbani kwako. Pia unaweza kuwekapesa kwenye akaunti yako kupitia KwikPay, M-PESA au Airtel Money. Kumbuka, daima hauwezi kupoteza tiketi yako ya kwanza ukiwa na Meridianbet, tuna Bonasi ya 100% inakusubiri.
Meridian - Nyumba yenye odds bora na bonasi kubwa!
No comments: