MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MKURANGA ULEGA ANATARAJIA URUDISHA FOMU LEO
MGOMBEA Ubunge jimbo la Mkuranga,Abdallah Hamisi Ulega anatarajia rasmi kurudisha fomu kesho baada ya udhamini ukamilika.
Akizungumza wilayani Mkuranga mkoani Pwani leo Agosti 24, 2020 baada ya kumaliza kujaza fomu Ulega amewashukuru wote waliomdhamini na kuahidi kutokuwangusha.
Aidha ametoa wito kwa wanachama wa Chama cha Mapindunzi kuhakikisha wanashiriki kampeni kikamilifu ili kuwezesha chama hicho kushinda kwa kishindo.
Pamoja na kuwashukuru waliomdhamini Ulega amewahidi kutowaangusha wanamkuranga na kuwataka kuendelea kudumisha umoja na ushirikiano ndani na nje ya chama.
Zaidi ya wadhamini mia 300 wamejitokeza kumdhamini Ulega huku wanaohitajika ni thelasini na moja tu.
Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga, Abdallah Hamisi Ulega (kushoto) akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapindunzi baada ya kumaliza kujaza fomu ya kugombea ambapo amewashukuru wote waliomdhamini na kuahidi kutokuwangusha, leo Agosti 24, 2020 wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
Wanachama wa Chama cha Mapindunzi wakimsikiliza Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga,Abdallah Hamisi Ulega (hayupo pichani)
Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga,Abdallah Hamisi Ulega akiwasalimia Wanachama wa Chama cha Mapindunzi.
Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga,Abdallah Hamisi Ulega akiwasalimia Wanachama wa Chama cha Mapindunzi.
Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga,Abdallah Hamisi Ulega (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Chama cha Mapindunzi (CCM) leo Agosti 24, 2020 wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
No comments: