Dkt. Allan Kijazi asisitiza umuhimu wa kupitia vema Miundo ya Taasisi za Uhifadhi
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi akisisitiza kuhusu umuhimu wa kupitia vema Miundo ya Taasisi za Uhifadhi ili kuliwezesha jeshi hilo kutenda kazi zake kiutaalam zaidi na kwa ufanisi mkubwa huku Taasisi za Uhifadhi zikizingatia kuimarisha Uhifadhi wa Wanyamapori na Misitu na kudhibiti ujangili. kikao hicho cha kujadili na kupitia Miundo ya Taasisi ( Organization Structure) ili kuendana na matakwa ya sheria iliyoanzisha Jeshi la Uhifadhi, kilichofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki, kimehudhuriwa na Makamishna wa Uhifadhi wa Taasisi za Uhifadhi za Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, Hifadhi za Taifa Tanzania, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania. Kushoto ni Mkurugenzi wa Wanyamapori Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Maurus Msuha.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro Kanali Martin Michael Kilugha (kushoto) na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi - Usimamizi wa Sheria na Mikakati ya Ulinzi na Usalama, John Nyamhanga ( kulia) wakifurahia jambo kufuatia michango ya wajumbe wa kikao cha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi na Makamishna wa Taasisi za Uhifadhi Tanzania, kilichofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.
Naibu Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Constantine Kanyasu, akiteta ma Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Adolf Mkenda wakati wa hafla fupi ya kutoa Nyota kwa Hoteli za Mkoa wa Dodoma zilizopangwa katika Daraja za Ubora. Hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma
Washiriki wa Mkutano wakifuatilia kwa umakini mkutano wa kupitia na kuhuisha Miundo ya Taasisi ili kuendana na matakwa ya sheria iliyoanzisha Jeshi la Uhifadhi. Mkutano huo ulioongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi, umefanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Kutoka kulia ni Kamishna wa Uhifadhi Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo, Naibu Kamishna wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara TANAPA, William Mwakilema na Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Huduma Saidizi Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Huduma Saidizi Emmanuel Wilfred. Picha na Woinde Shizza
No comments: