WAJASIRIAMALI JIJINI MWANZA WAPATIWA MAFUNZO YA KUFIKIA VIWANGO VYA BIDHAA ZAO

Na Abdullatif Yunus Michuzi Tv
Wajasiriamali na wafanyabiashara wanaojihusisha na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali Jijini Mwanza, Baadhi yao wamekuwa  miongoni mwa wanufaika wa Semina ya Mafunzo ya kufikia Matakwa ya Viwango iliyoratibiwa na TBS Jijini humo.

Shirika la Viwango Nchini TBS limeendeleana Semina hiyo Jijini Mwanza  baada ya kumaliza Semina Kama hiyo Karagwe na Geita, ambayo ni Maalum kwa ajili ya kutoa uelewa zaidi Juu ya maeneo ambayo yamewaletea changamoto katika kukidhi Matakwa ya Viwango. 

Wajasiriamali wengi Nchini wameonekana kupata changamoto katika uzalishaji na usindikaji wa bidhaa zao hasa katika kukosekana kwa elimu Juu ya Vifungashio na ufungashaji wa bidhaa husika, na hata wanapofungasha ni maneno gani au Taarifa zipi wanatakiwa kuziweka katika kifungashio hicho, ikiwa ni sambamba na suala la utunzaji wa kumbukumbu za udhibiti wa ubora wakati na Baada ya uzalishaji.

Kupitia changamoto hizo Tayari TBS imekuwa ikitoa wakufunzi mbalimbali wanopita kwa Wajasiriamali hao kuwapa mada zinazohusu maeneo niliyotaja ambayo ndizo changamoto hasa, na hivyo kupitia Semina hizo  tayari maelfu ya Wajasiriamali wamenufaika na bidhaa zao, na wengine wakiwa katika hatua za kupewa alama ya ubora baada ya kuhakikiwa na Shirika la Viwango.
Mkuu wa Wilaya Ilemela Dkt. Severine Lalika akitoa Hotuba yake kwa washiriki wa Semina ya Mafunzo yaliyotolewa na TBS Jijini Mwanza katika ukumbi wa SIDO Wilayani Ilemela.
Mkaguzi Ubora kutoka TBS Kanda ya Ziwa Ndg. Nelson Mugema, akitolea ufafanuzi baadhi ya maswali yaliyoulizwa na washiriki wa Semina ya Mafunzo yaliyotolewa na TBS Jijini Mwanza katika ukumbi wa SIDO Wilayani Ilemela.
Afisa Viwango toka TBS , Zena Issa akizidi kudadavua mada wakati wa Semina ya uwezeshi kwa Wajasiriamali kufikia matakwa ya Viwango Jijini Mwanza.
Meneja Mafunzo na Utafiti, Hamisi Sudi kutoka TBS akiwasilisha Hotuba ya Mkurugenzi Mkuu TBS mbele ya Washiriki na Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya  llemela.
Picha ya Pamoja ya Washiriki wa Semina ya Mafunzo Wezeshi ya Wajasiriamali wakiwa na Mgeni rasmia Mkuu wa Wilaya Ilemela Dkt. Severine  Lalika aliyevaa tai

No comments: