TAKUKURU ARUSHA YAOKOA SHILINGI BILIONI 1.7 ZA KODI YA SERIKALI,VYAMA VYA USHIRIKA


Na Woinde Shizza,ARUSHA


TAASISI ya Kupambana na Kuzuia  Rushwa(TAKUKURU)Mkoa wa Arusha imeokoa zaidi ya shilingi bilioni 1.7 za kodi ya Serikali pamoja na fedha za vyama vya ushirika  ,fedha ambapo zimepatikana baada ya operesheni  mbalimbali zilizofanywa  na taasisi hiyo kwa kipindi cha mwezi April hadi Juni 2020.

Pia waliweza kufanikiwa kuokoa jumla ya shilingi 190163,850 za wajasiriamali  sita wa Jiji la Arusha walizokuwa wamezulumiwa na wamiliki wa kiwanda cha Kijenge Animal Products Limited .

Akizungumza na waaandishi wa habari Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Arusha  James Ruge amesema kuwa  wamefanya operasheni mbalimbali na kufanikisha kurejesha kodi ya Serikali  iliyokuwa haijalipwa na kampuni ya kitalii ya uwindaji ya Eshkesh Safari pamoja na fedha za chama cha ushirika cha ACU (Arusha Coperative Union)zilizokuwa hazijalipwa kwa chama baada ya mauzo ya mali za ushirika jumla ya shilingi 1,764,808,176.

“Ilikuhakikisha fedha hizo zilizokuwa sza mauzo ya mazao ya wajasiriamali hao yaliyopokewa na kiwanda hicho tangu January 2020 takukuru Arusha imeendelea na uchunguzi huu kiasi kilichosalia nii shilingi 99,097,453 na fedha hizi zinaliwa na watuhumiwa  ndani ya mwezi mmoja  ambapo Michael Mtana  Sh.50,725,450,Issa Mush Sh. 53,258,00,Keneth  Lauwo Sh.19,639,200,Gregory Mukabi sh.34,125,760,Leo Marandu sh 28,793,040 pamoja na  Ahamed Mavura Tsh 13,622,400,"amesema Ruge

Amesema kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 1.4 ni kodi ya Serikali ya mizigo mbalimbali ambayo ilikuwa haijalipwa na kampuni ya uwindaji na utalii ya Eshkeshi ya jijini Arusha ,kiasi cha shlingi zaidi ya milioni 200 ni sehemu ya shilingi milioni 900.4za chama kikuu cha ushirkia cha ACU ilizokuwa zimefanyiwa ubadhirifu baada ya mali za chama hizo kuuzwa kwa watu wasio waaminifu.

Wakati Sh.milioni 45,448,140 zilikuwa ni fedha za vyama vya msingi vya  ushirika  ,posho zilizolipwa zaidi ya stahili na fedha za makusanyo ya halmashauri ambazo hazikuwasilishwa  kwenye akaunti za halmashauri husika .

Amesema vyama vya msingi vya ushiria na Saccos wialya za Arumeru ,Karatu na Longido ni kiasi cha shilingi 37,745,640  makusanyo ambayo hayakuwasilishwa benki ni shilingi 1,652,500 ,huku posho zilizorejeshwa baada ya kulipwa isivyostahili ikiwa ni shilingi 6,050,000 ambapo amebainisha kuwa mbali na kufanikisha hilo.

Pia amesema  Takukuru mkoa wa Arusha imeendelea kutekeleza majukumu yake ya sheria kwa kutumia njia kuu tatu ambazo ni uchunguzi na mashtaka ,uelimishaji wa umma na utafiti na uthibiti huku  ikiwashirikisha  wadau mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha kwamba madhara ya rushwa yanaeleweka vyema kwa jamii hivyo kuiwezesha jamii kutambua umuhimu wa kila mmoja wao kushirki katika mapambano  dhidi ya rushwa.

Katika tukio lingine TAKUKURI imefanikiwa kumrejeshea mfanyabiashara Advera Kyaruzi fedha kiasi cha shilingi 5,480,00 ambayo ni sehemu ya jumla ya shilingi milioni 15m alizokuwa amedhuluiwa na wafanyabiashara wenzake Gervas Andera Mollel na Joseph Chirstopher Molle tangu mwaka 2018 ili kuhakikisha fedha ambazo zilikuwa ni za mzigo wa baiashara ulizotapeliwa na Hervas na wenzake.

Hata hivyo TAKUKURU Mkoa wa Arusha  inaendelea na uchunguzi kuhakikisha fedha zilizobaki zinali0pwa na watuhumiwa. Aidha alisema wamejenga mikakati  madhubuti katika kuendelea na mapambano dhidi ya rushwa hasa katika kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais ,wabunge na madiwani uliopangwa kufanyika mwezi Oktoba 28,mwaka huu.

Pia wameweka lengo la kuendelea na mikakati ni kuhakikisha kuwa wanatekeleza majukumu yao  makuu matatu ambayo ni kuelimisha ,kuzuia na kupambana na rushwa kwa ufasaha ili kuweza kufikia lengo la kuwa na utawala bora nchini na kuitokomeza rushwa kabisa.

Akizungumzia mchakato wa kura za maoni zilizofanywa na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) amesema “Katika kipindi cha uchaguzi wa kura za maoni za CCM tumeweza kukamata wagombea zaidi ya 20 ambao tunaendelea na uchunguzi zidi yao mmoja wapo ni Philemon Molle.

"Pia kunataarifa zilikuwa kwenye mitandao kuwa tumemkamata na Mrisho Gambo ,naomba nifafanue hatujamkamata wala hatujamuita hapa ofisini kwetu kuhojiwa ila kunamalalamiko yalillletwa na tunaendelea kuyafanyia uchunguzi na ukikamilika kwa wote na kubainika kuwa walihusika sheria itachukua mkondo wake.

"Sisi hatufanyi kazi kwa kufata maelekezo ya mtu yeyote bali tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria zetu zinavyotuelekeza hatuwezi kufanya kazi kwa kufata mitandao ya kijamii wala mtu yeyeto yule, “alisema Ruge

Aidha ametoa rai kwa vyama vya siasa vyenye nia ya kusimamisha wagombea katika uchaguzi mkuu ujao kuhakikisha kuwa wagombea watakaowasimamisha kuwania nafasi mbalimbali wana sifa stahili ili kuwapa wapiga kura urahisi wa kuchagua  kiongozi bora  pasipo kurubuniwa na rushwa.

Pia watia nia na wagombea wote wanaaswa kufuata sheria,kanuni na utaratibu na kujiepusha kumumia rushwa kushawishi  kuteuliwa au kuchaguliwa kwani watakapobainika  TAKUKURU  haitasita kuchukua hatua kali dhidi yao .

No comments: