CHUO KIKUU MZUMBE YAENDELEA KUWANOA WATAALAMU WA UGAVI NA MANUNUZI


Mkuu wa Kampasi ya Dar es Salaam ya  Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Honest akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa Ugavi na Manunuzi kutoka taasisi za Umma, Taasisi Binafsi, Wanafunzi pamoja na Wakufunzi.


CHUO Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar Es Salaam yaendelea kuwanoa wataalamu wa Ugavi na manunuzi.

Ni Chuo kinachoe kutoa elimu ya mabadiliko ya kiuongozi katika sekta ya Ugavi na manunuzi, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuuna  Mzumbe na Mratibu wa  Mradi wa Kuehne, Daktari Omary Swalehe  amesema kuwa mabadiliko ya Teknolojia ni makubwa hivyo wataalamu wa Ugavi na Manunuzi nao lazima waendane uelekeo wa Teknolojia.

Dkt.Omary amesema kuwa wateja wanabadilika sheria, mifumo pamoja na kanuni nazo zinabadilika ni mhimu na wataalamu wa Ugavi na manunuzi  kubadilika pia.

"Wateja ndio wanaamua wanataka nini,wanahitaji bidhaa gani kwahiyo Kampuni lazima zijue mahitaji ya wateja wao kuendana na Teknolojia inavyo elekea." Amesema Dkt. Omary

Hata hivyo amesema kuwa taasisi na wataalamu lazima wabadilishe mtazamo wako katika masuala mazima ya Ugavi na Manunuzi.

Kwa upande wake Mkuu wa Kampasi ya Dar es Salaam ya  Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Honest Ngowi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya wataalamu wa ugavi na manunuzi katika Chuo Kikuu Mzumbe jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa mambo mengi yanakwenda kidijitali hivyo walaji wengi wamehamia Mtandaoni. 

"Walaji na Wateja wengi wananunua bidhaa mtandaoni, iwe mziki, nguo na vitu mbalimbali kwa hiyo haya Kampuni za ugavi na manunuzi pamoja na wataalamu ni mhimu kubadilika kuendana na mahitaji ya wateja ". Amesema Profesa Ngowi.

Licha ya hili Profesa Ngowi  amesema kuwa  Chamoto kubwa kampuni zishindwa huendana na mabadiliko ya Teknolojia hivyo amewaasa kuw waweze kuendana na mabadiliko hayo ili kufanya biashara na wateja wanaobadilika na mfumo wa manunuzi.

Wito umetolewa kwa wataalamu wa ugavi na manunuzi pamoja na kampuni mbalimbali kuendana na mabadiliko ya uongozi na teknolojia inakoelekea.

Wataalamu waliopata mafunzo ya mabadiliko ya mfumo wa uongozi katika Ugavi  na Manunuzi ni kutoka Taasisi za Seikali, Taasisi Bianafu, Taasisi za elimu pamoja na wanafunzi wanaosoma masuala ya Ugavi na manunuzi.

Kwa Upande wake  Mwakilishi Mkazi wa taasisi la Kuehne Foundation, Betrice  Milu,  amesema kuwa taasisi ya Kuehne wanafanya kazi ya kusaidia Wakufunzi pamoja na wataalamu wa masuala ya manunuzi na ugavi hapa nchini kubadilika na kuendana na teknolojia.

Amesema kuwa wameshafanya semina mbalimbali kwaajili ya kuwajengea uwezo wadau wa ugavi kwani kumekuwa na mafanikio makubwa kwani washiriki wanajitokeza kwa wingi.

"Katika kushirikiana na Chuo Kikuu Mzumbe tumeona ushiriki umekuwa mzuri kwani tumepata washiriki wengi na mafunzo yanaonesha mlengo chanya katika masuala mazima ya Mabadiliko katika Manunuzi na Ugavi." Amesema Beatrice.
 Mkuu wa Kampasi ya Dar es Salaam ya  Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Honest  Ngowi akizungumza wakati wa kufungua mafunzo ya wataalamu wa Ugavi na Manunuzi juu ya mabadiliko ya kiteknolojia katika sekta ya Ugavi na Manunuzi jijini Dar  Es Salaam leo.
 

  
 Baadhi ya Wataalamu wa Ugavi na Manunuzi wakiwa kwenye Mafunzo ya Mabadiko ya Kimfumo wa Uongozi katika Ugavi na Manunuzi.
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya Mabadiliko ya Kimfumo katika Ugavi na Manunuzi jijini Dar es Salaam leo.
 Mkufunzi, Bosco Mapunda akichangia Mada katika Mafunzo yaliyofanyika Kampasi ya Dar es Salaam ya Chuo Kikuu Cha Mzumbe leo.

No comments: