BODI YA MIKOPO YATOA ELIMU KWA WANAFUNZI WANAOTARAJI KUIJIUNGA NA ELIMU YA JUU MKOANI GEITA



Maafisa kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi ya Elimu ya Juu (HESLB) wakizungumza na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Geita, Isaya Busagwe (katikati) wakati walipofika shuleni hapo kutoa elimu kuhusu mwongozo wa utoaji mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka 2020/2021 yaliyoendeshwa na HESLB kwa wanafunzi waliohitimu masomo ya kidato cha Sita  na Stashahada Mkoani Geita. Mafunzo hayo yalifanyika jana Jumatatu (Julai 27, 2020). Kushoto ni Meneja wa HESLB Kanda ya Ziwa, Ussama Choka.
Wanafunzi wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Kilangalala iliyopo Mkoani Geita wakinawa maji kwa kutumia vitakasa mikono muda mfupi kabla ya utoaji elimu kwa umma kuhusu mwongozo wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya Juu kwa mwaka 2020/2021 kwa mwaka 2020/2021 yaliyoendeshwa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa wanafunzi waliohitimu masomo ya kidato cha Sita na Stashahada yaliyofanyika katika Shule ya Sekondari Geita Mkoani Geita jana Jumatatu 
Afisa Elimu (Taaluma) Mkoa wa Geita, Kaitila Mafwimbo akizungumza na wanafunzi wa Shule za Sekondari za Kalangalala na Geita pamoja na waliohitimu masomo hayo wakati utoaji elimu kuhusu mwongozo wa utoaji mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka 2020/2021 yaliyoendeshwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kwa wanafunzi waliohitimu na wanaondelea na masomo ya kidato cha Sita na Stashahada Mkoani Geita. Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Shule ya Sekondari Geita Mkoani Geita jana Jumatatu
Meneja Mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Kanda ya Ziwa, Ussama Choka akizungumza na wanafunzi wa Shule za Sekondari za Kalangalala na Geita waliosoma kidato cha sita na wale waliohitimu masomo hayo wakati utoaji wa elimu kuhusu mwongozo wa utoaji mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa wanafunzi waliohitimu na wanaondelea na masomo ya kidato cha Sita pamoja na Stashahada. Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Shule ya Sekondari Geita Mkoani Geita
Baadhi ya wahitimu wa kidato cha sita kutoka katika Shule mbalimbali Mkoani Geita wakifuatilia kwa makini mafunzo ya elimu kwa umma kuhusu mwongozo wa utoaji mwa wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka 2020/2021 kwa wanafunzi waliohitimu na wanaondelea na masomo ya kidato cha Sita pamoja na Stashahada yaliyotolewa na Maafisa kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi ya Elimu ya Juu (HESLB). Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Shule ya Sekondari Geita Mkoani Geita

No comments: