ALIYEKUWA AKISOTEA MAFAO YAKE TANGU MWAKA 1997 TANITA ATOA KILIO CHAKE KWA RAIS DKT. MAGUFULI... APATA TUMAINI, ULEGA APEWA JUKUMU
Na Said Mwishehe, Michuzi TV.
NAIBU Waziri wa Mifugo na aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega amepewa maelekezo na Rais Dk.John Magufuli kuhakikisha anamsadia mwana mama anayeishi wilayani Mkuranga aliyekuwa akifanya kazi TANITA jijini Dar es Salaam na kisha kusotea mafao yake tangu 1997.
Rais Magufuli akiwa katika eneo la Mkuranga ambako alisimama kusalimiana na wananchi akiwa safarini akitokea mkoani Mtwara pamoja na malalamiko mbalimbali ya wananchi, mama huyo alisema alikuwa akifanya kazi TANITA na tangu mwaka 1997 amekuwa akisumbuka kupata mafao yake.
"Mheshimiwa Rais, kila tukienda tunaambiwa kesho keshokutwa, kwenye ofisi yako faili letu limefika, kwa Waziri Mkuu tumekwenda lakini hadi leo bado, hatujafaniki.Juzi juzi tumeeda pale Hazina , tukaambiwa waende viongozi wetu, wamefuatilia,"amesema mama huyo.
Kutokana na maelezo ya mama huyo,ndipo Rais wakati anatoa ufafanuzi wa kero mbalimbali za wananchi hao, ndipo alipoanza kuzungumza suala hilo la mafao yake ambapo alisema "kuhusu lile la TANITA, nenda kwa Mkuu Mkoa wa Dar es Salaam.
"Au nenda mahakamani, kamshtaki huyo mwajiri wako, basi kama limeshafika hazina nenda kwa Waziri wa Fedha, Mbunge(Ulega) kesho mbebe huyu mama mpeleke kwa Waziri wa Fedha, umpakie kwenye gari lako. Kwingine kote kunakohusika mtembeze, TANITA nenda naye kwanza hawawezi kukusingiza unampenda , huyu mama amekuzidi umri.
"Kesho akubebe akupeleke TANITA akutoe pale kama ishu iko Wizara ya Fedha nenda naye na kisha umrudishe hapa, na hela ya kumlisha Dar es Salaam uumpe,"amesema Rais Magufuli.
No comments: