WACHEZAJI WA MASHINDANO YA DIPLOMATIC GOLF’ WAMUAGA MKURUGENZI MKAAZI WA WFP
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ndumbaro akimkabidhi Mkurugenzi mkaazi wa (WFP) Bw. Michael Dunford moja kati ya zawadi zilizoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ndumbaro akiagana na Mkurugenzi mkaazi wa (WFP) Bw. Michael Dunford
Mkurugenzi mkaazi wa (WFP) Bw. Michael Dunford akipokea moja kati ya zawadi zilizoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ndumbaro
Wachezaji wa Mashindano ya Diplomatic Golf wakiwa katika picha ya pamoja katika viwanja vya gymkhana leo jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi mkaazi wa (WFP) Bw. Michael Dunford akicheza golf katika viwanja vya gymkhana leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro akicheza golf katika viwanja vya gymkhana leo jijini Dar es Salaam*********************************
Wachezaji wa Mashindano ya Diplomatic Golf mchezo ambao unaoratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, wamemuaga mchezaji mwenzao ambae pia ni Mkurugenzi mkaazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Bw. Michael Dunford.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro, amebainisha hayo wakati walipokuwa wakifanya mazoezi pamoja na wachezaji wengine akiwemo, Mkurugenzi mkaazi wa (WFP) Bw. Michael Dunford leo katika viwanja vya gymkhana jijini Dar es Salaam.
Tumekutana Jijini Dar es Salaam, kumuaga mcheza mwenzetu Michael Danford gofl ambaye anakwenda Nairobi kikazi……. limekuwa pambano kali lakini tumemaliza salama.
Pia tutakuwa na fursa ya kumpa zawadi zilizoandaliwa na wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na washindi wengine.
Mchezo wa leo ulikuwa mahsusi kwa ajili ya kumuaga Bw. Michael Dunford ambaye amemaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini ambapo kwa sasa amepangwa kikazi katika nchi jirani ya Kenya.
“Diplomatic Golf, ni fursa mahsusi kwa mawaziri, wabunge, wanasiasa, wanadiplomasia na wananchi wote wa kawaida kukutana na kubadilishana uzoefu wa mchezo huo na kutengeneza njia mbadala ya kuikuza tasnia hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wapenda golf,” Amesema Dkt. Ndumbaro.
Kwa upande wake, Mkurugenzi mkaazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Bw. Michael Dunford amesema kuwa mchezo ulikuwa mzuri na wakufurahisha.
“Mchezo wetu wa leo ulikuwa mzuri sana na wakufuraisha…..mimi pamoja na Naibu Waziri, Dkt. Ndumbaro tumepata alama sawa,” Amesema Bw. Dunford
Mwaka 2019, Mashindano ya Diplomatic Golf yalifanyika visiwani Zanzibar katika Viwanja vya Zanzibar Golf Course Sea Cliff, ambapo mwaka huu yanatarajiwa kuwa tofauti huku vitu vingi vikiwa vimeboreshwa zaidi.
No comments: