NAIBU WAZIRI MABULA ATAKA UPIMAJI MAENEO YA MIGODI KUEPUKA MIGOGORO
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akioongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel (Kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Geita Josephat Maganga kuelekea kuzungumza na watendaji wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Geita wakati wa ziara ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi mwishoni mwa wiki.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Geita wakati wa ziara ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Geita Josephat Maganga na kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Geita Rugambwa Banyikila
Baadhi ya Watendaji wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Geita awakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati wa ziara ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi mwishoni mwa wiki.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiingia kukagua jengo la Ofisi ya Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) Biharamulo mkoa wa Geita lililojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wakati wa ziara yake katika mkoa wa Geita mwishoni mwa wiki.
Taswira ya jengo la Ofisi ya Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) Biharamulo mkoa wa Geita lililojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Chato, Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu na watendaji wengine mbele ya jengo la Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) Biharamulo mkoa wa Geita wakati wa ziara yake katika mkoa ho mwishoni mwa wiki. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
……………………………………………………………………………………………………..
Na Munir Shemwta, WANMM GEITA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amezitaka halmashauri nchini kupitia idara zake za ardhi kuhakikisha zinapima maeneo yote yenye migodi ili kuondokana na migogoro.
Dkt Mabula alisema hayo mwishoni mwa wiki aipozungumza na watendaji wa sekta ya ardhi kwenye mkoa wa Geita akiwa katika ziara ya kukagua utendaji wa sekta ya ardhi pamoja na utekelezaji wa miradi inayofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mkoa humo.
Dkt Mabula alisema, mkoa wa Geita una migodi mingi bila kuwa na suala la upimaji na umilikishaji maeneo ya Migodi migogoro kwenye maeneo hayo haitaisha kwa kuwa leseni ya uendeshaji shughuli za uchimbaji madini inaonesha umiliki eneo la chini lenye madini.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alitolea mfano wa Mgodi wa Madini wa Nyamongo kuwa, umefanikiwa kupima maeneo yake na sasa mgodi huo pamoja na kuwa na haki ya umiliki eneo la chini la madini (mineral rights) lakini Mgodi huo inamiliki pia eneo la juu (surface rights) na hivyo kuondokana na migogoro.
‘’Hakikisheni wanaoendesha shughuli za migodi wanamiliki kihalali maeneo yao, ana surface rights na ana minerals rights ili awe salama habari ya kufukuzana na watu wanaopita juu haipendezi, ana haki ya kuwa pale juu kwa sababu wewe leseni yako ni ya kule chini sasa wewe unaniondoaje’’ alisema dkt mabula
Kwa mujibu wa Dkt Mabula, kwa bahati nzuri kwa sasa wachimbaji wadogo nao tayari wameanza kuanishiwa maeneo hivyo kasi ya kuyapima maeneo hayo iongezeke ili wanaoendesha shughuli za migodi wamiliki kihalali maeneo yao sambamba na kuongeza wigo wa makusanyo ya kodi ya ardhi kwa serikali.
Amewataka watendaji wa sekta ya ardhi katika maeneo yenye migodi kuangalia namna bora ya kuzungumza na wamiliki hao ili kutambua umuhimu na faida ya kupima maeneo yao kwa lengo la kuondokana na mgogoro.
Akiwa katika wilaya ya Chato ambako alikagua pia mradi wa ujenzi wa ofisi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Biharamulo unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dkt Mabula ameitaka wilaya hiyo kuandaa mpango wa mji huo ili kuwa na sura ya kitalii na kusisitiza utolewaji elimu kwa viongozi wa vijiji kuwaelekeza wananchi umuhimu wa kujenga nyumba kwa mpangilio ili kuepuka ujenzi holela
Naibu Waziri Mabula aliwataka watendaji wa sekta ya ardhi katika wilaya ya Chato kufuatilia wananchi wasijenge kiholela na kubainisha kuwa NHC inaweza kutumika katika kupanga miji kupitia ujenzi wa nyumba zake ili kuzuia ujenzi holela.
No comments: