RC MAKONDA AWATAKA UVCCM KUSIMAMA KIDETE KUKIPIGANIA CHAMA CHA MAPINDUZI.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewataka Vijana wa Chama cha Mapinduzi kukilinda Chama hicho na kuwa mabalozi wazuri wa kuyaeleza maendeleo yaliyofanywa na Rais Dkt. John Maguguli katika kipindi cha Miaka Mitano.

RC Makonda ametoa kauli hiyo wakati wa Kikao na Vijana wa UVCCM Mkoa wa Dar es salaam ambapo amesema yapo Maendeleo Makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano na kama wasipoyazungumzia watatoa mwanya kwa watu wasiolitakia mema Taifa kupenyeza Wongo.

Aidha RC Makonda amewataka Vijana hao kuwa macho hususani kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu kwakuwa wapo baadhi ya watu wenye tamaa watakuwa tayari kuvunja hata Amani ili tu wapate fedha za kushibisha matumbo yao.

Pamoja na hayo RC Makonda amesema ifikapo Juni 20 ataanza ziara na Kamati ya Siasa ya Mkoa kwa lengo la kukabidhi kwa Chama miradi yote iliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya Tano chini ya Uongozi imara wa Rais Magufuli.

Hata hivyo RC Makonda ametoa Msaada wa Mabati na Mbao za kupaua kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa Ofisi ya UVCCM Wilaya ya Kigamboni.
 

No comments: