KAILIMA ATEMBELEA OFISI ZA CHAMA CHA WAFUGAJI TANZANIA (CCWT) DODOMA KUONA MWENENDO WA MAANDALIZI YA UCHAGUZI WA CHAMA HICHO
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima, akitoa maelekezo ya Serikali kwa Viongozi wa Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT) hawapo pichani, baada ya kukuta Ofisi zao zikiwa zimefungwa na hakuna maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Chama hicho. Kailima, ameelekeza Wanachama wote wanaotaka kushiriki kwenye Mkutano wa kuchagua Tume ya Uchaguzi utakaofanyika 25 Juni, 2020 wakalipe ada zao na kuwasilisha Stakabadhi katika Ofisi ya Chama hicho. Taarifa hiyo ameitoa kwenye Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima, akitoa maelekezo ya Serikali kwa Viongozi wa Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT) hawapo pichani, baada ya kukuta Ofisi zao zikiwa zimefungwa na hakuna maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Chama hicho. Kailima, ameelekeza Wanachama wote wanaotaka kushiriki kwenye Mkutano Mkuu wa kuchagua Tume ya Uchaguzi utakaofanyika 25 Juni, 2020 wakalipe ada zao na kuwasilisha Stakabadhi katika Ofisi ya Chama hicho. Taarifa hiyo ameitoa kwenye Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima, akiwaonyesha waandishi wa habari Ofisi za Viongozi wa Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT), ambazo zilikuwa zimefungwa na hakuna maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Chama hicho. Kailima, ameagiza Viongozi wa Chama cha Wafugaji Tanzania waliopo madarakani wahakikishe wanasimamia na kutekeleza Katiba yao na Sheria ya Chama hicho. Taarifa hiyo ameitoa kwenye Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dodoma.
Afisa Sheria Ofisi ya Msajili wa Jumuiya za Kijamii wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Eliud Mwailafu (Wa kwanza kushoto) akitoa taarifa ya Kamati inayoratibu Uchaguzi wa Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT) kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima (hayupo pichani) kuhusu mwenendo wa Maandalizi ya Uchaguzi wa Chama hicho, jijini Dodoma.
Mlango wa Ofisi ya Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT) ambao ulikutwa umefungwa baada ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima na kamati inayoratibu uchaguzi wa Chama hicho kutembelea ofisi hizo zilizopo Hotel Fifty Six kuona mwenendo wa maandalizi ya Uchaguzi wa Chama hicho na kukuta Ofisi hizo zikiwa hazijafunguliwa na Viongozi waliokuwepo madarakani hawapo, leo 13 Juni, 2020 jijini Dodoma
No comments: